Mbishi 4 real
JF-Expert Member
- Jan 16, 2014
- 640
- 655
Kwa kawaida tunapokua tumeingia kwenye mahusiano ya kimapenzi na wanawake huwaga tunapeana namba zetu zote za simu za mitandao tofauti tofauti ili ikitokea mpenzi wako kakukosa hewani kwenye namba flani basi awe na uwezo wa kukupata kwa namba nyingine ambayo inawezekana isifahamike na watu wengi lakini mpenzi wako hawezi kukosa kukupatia hiyo namba.
Inapotokea mmeachana asilimia kubwa ya wanaume ndio wanaoongoza kwa kufuta namba za wapenzi wao walioamua kuachana nao, mara nyingi huwa tunawaelekeza kabisa wanawake kwamba "futa namba zangu zote za simu" ili tu kuepusha usumbufu unaoweza kujitokeza.
Suala hili limekua tofauti kidogo kwa upande wa wanawake ambapo unaweza kumwambia afute namba zako za simu akakujibu "sawa" lakini asifanye kama vile ambavyo umemtaka afanye.Wanawake walio wengi wana uwezo wa kukariri namba za simu kwa haraka sana kuliko kitu chochote na hata kama akizifuta bado atakua na uwezo wa kukutumia sms na kukupigia pindi anapojiskia kufanya hivyo hata kama ulishamkataza.
Hii inatokana na nini ? je ni upendo wa dhati alionao juu yako hata kama umemuacha au ni ulimbukeni tu wamapenzi ?
Karibuni tuambizane