Kwanini wanaume wanatongoza mabinti wenye umri mdogo?

Kwanini wanaume wanatongoza mabinti wenye umri mdogo?

magode

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2014
Posts
2,204
Reaction score
3,339
Hivi mwanaume mtu mzima wa zaidi ya miaka 45,unatongoza binti mwenye miaka 16,17 au hata 22. Unakuwa umefikiria nini hasa, hivi watoto wa umri huo si watoto wako hao.

Mwanaume mwenzangu unapata wapi ujasiri wa kuvua nguo mbele ya mtoto kama huyo,kuna mzee ana zaidi ya miaka 48 ana msumbua binti anayenisaidia kazi zangu hapa,binti ana miaka 19. Kibaya zaidi huyu binti kazaliwa hapa na huyu mzee akiona.

Binti ameshaleta malalamiko kwangu zaidi ya mara 4 nikalazimika kuongea na yule mzee kirafiki,maana hata me ananizidi umri mzee yule alionyesha kunielewa na kuniomba nimtunzie heshima nami nikamuondoa shaka.

Leo binti kanionyesha message za yule mzee,nimechoka kabisaa,nimekubaliana na mawazo ya binti ya kuzipeleka hizi message kwa mkewe na watoto wake. Au nimekosea wadau.
 
Ngoja kidogo atakuji mwnyw maana hum yumo nikiona kimya nitajibu maana mcba wa komba ni pigo la ccm
 
Ingekuwa mm badala ya kulia lia hapa ningeenda kupachimba..chukua hatua..tangaza vita..mwanzoni atakuchukia lkn heshima itakuja..
 
Last edited by a moderator:
amu

Mkuu amu mbona hiyo mbinu ndo alianza nayo,ofisini tunafanya biashara hizo ulizotaja,tigopesa,mpesa nk. Ilikuwa akija kutoa au kuweka lazima amuachie elf 10 au 5000 za soda. Mwanzo Binti alikuwa anazichukua,lkn alipomtongoza,akagoma kuzipokea. Naweza kusema ni mmoja wa mabinti wanaojiheshimu kwa karne hii.
 
Last edited by a moderator:
Ni jambo la hatari sana kuruhusu hisia zetu zitutawale na kutuongoza pasi na kutumia akili hata chembe katika ulimwengu wa hisia unaweza ukamfananisha paka na simba na kuanza kutimua mbio na watu wanaanza kukushangaa,hata paka naye atakushangaa,watu wa aina hiyo hujiona wapumbavu sana wakitoka katika ulimwengu wa hisia na kuja katika uhalisia wenyewe.

Huyo mzee bahati mbaya anatumia hisia zaidi za ngono kuliko uhalisia wenyewe,katika ulimwengu wake wa hisia anaona ni sahihi kwani yeye anamtazama huyo binti kama mwanamama mtu mzima anayestahili kupata kile anachotaka kumpa,wakati nyinyi mkimshagaa kwa kile anachotaka kukifanya kwa kuwa sio sahihi kiuhalisia kwani huyo binti analingana na mabinti zake kama sio wajukuu zake na yeye pia anawashangaa nyie kwani haoni ubaya wowote yeye katika lile analotaka kulifanya.

Hapo inatakiwa busara itumike.Mimi sikushauri umpelekee hizo sms mkewe..bali unatakiwa umpelekee wewe ukiwa na huyo binti huku ukimsisitizia kuwa analotaka kulifanya sio zuri kwani linaweza kumvunjia heshima yake.Ukimpelekea mkewe hizo sms unaweza kuisambalatisha familia yake na kuleta majuto kwa watu wengine wasio na hatia kwani ndoa nuingi zimekaa kimitego mitego tu huku zikisubiri sababu tu zivunjwe.
 
Mzee ndo kaona size yake hiyo sa we unataka kumchagulia size ebo!
 
KikulachoChako

Salute kwako mkuu KikulachoChako yaani ni jambo la kusikitisha kwakweli,ukimuona huyo mzee humdhanii! Halafu ni mlokole anaabudu kwa mchungaji mmoja ambae hivi karibuni aliingia kwenye kashifa ya kuvuruga ndoa ya mwimbaji maarufu wa injili.
 
Last edited by a moderator:
Ukishakuwa mzazi hakuna kuona aibu, hata kama huyo mzee ashamaliza sio sawa aeendelee kumaliza anavyojisikia. Na binti naye anatakiwa ajue anafanya kosa kama shaanzana na huyo mzee. Kuumbuka mapema ni bora kabla mambo hayajaharibika zaidi. Mzaz hatakiwi kuona aibu katika malezi ya watoto hata kama sio wake wa kumzaa.
Mumba Daly
 
Last edited by a moderator:
Chunguza vizuri kwanza usije wewe ukaingia kwenye kashifa za house girl. Hiyo namba ya simu ya msichana wako aliipataje huyo mzee. Je binti ana hatari yoyote ya kuweza kubakwa au physical harassment. Ni vizuri pia uka consult wanasheria uone kama mazingira ya kumstaki yapo, otherwise unaweza kumchafulia jina bila sababu.
Huyo mzee ni wa Tanga?
 
Mpumbavu sana,unaanzaje kumtunzia mtu heshima ilhali yeye kashindwa kutunza heshima yake mwenyewe? kha! kamuumbue tu kwa kweli bazazi huyo
 
Back
Top Bottom