Kwanini wanashauri usivute gari lenye Automatic Gearbox ukipata break down, badala yake upakie kwenye Flatbed Truck

JituMirabaMinne

JF-Expert Member
May 4, 2020
3,327
9,328
Huu uzi nilitamani ningepata Automatic Gearbox mbovu nikaufanyia video. Kwa maana ninaamini kwa njia hiyo wote mngenielewa vizuri. Hata hivyo nitajitahidi kuelezea kwa kadri nitakavyoweza.

Hebu iangalie hii picha vizuri. Hii ni cross section ya Gearbox ya automatic. 99% gearbox za automatic zipo hivi. Iangalie vizuri Oil pump ipo tu baada ya Torque Converter.

Transmission-Altogether-1.jpg


Kwenye gearbox ukizima gari, Gearbox Oil inabakia maeneo mawili tu.

1. Kwenye torque converter.

2. Kwenye Sump ya Gearbox.

Sasa ipo hivi, unapovuta gari lenye automatic gearbox, engine inakuwa imezima, torque converter na Oil pump pia vinakuwa havizunguki. Hivi vitu huwa vinazunguka tu kama engine inazunguka.

Then Oil pump hazunguki, sehemu ya gearbox iliyobakia inazunguka bila Oil. Hivyo ni rahisi kuharibu gearbox.

Kuna baadhi ya gari mfano baadhi ya matoleo ya mercedes Benz gearbox inakuwa na secondary Oil pump na inakuwa na Tow mode(hii naomba isichanganywe na ile tow mode ya kuvuta trailer n.k.).

Hiyo secondary pump inakuwa activated utakapotaka kulivuta gari lako kwa ajili ya kusupply oil kwenye gearbox.

Ndio maana ukipata breakdown ushauri wa kwanza ita flatbed truck pakia au tow truck kama gari yako si AWD na mtanyanyua upande ambao ndio unadrive.

Na kama utaamua kuivuta gari yako basi fuata sheria hii.

1. Vuta kwa speed ndogo kwa kadri itakavyowezekana.
 
Hata gari manual haishauriwi sana kitaalamu kuivuta (towing). Diff kwa kawaida haipendi mzunguko unaoanzia kwenye matairi. Ndio sababu trucks kabla ya kuwa towed lazima ukate propeller shaft na uondoe drive shafts (axles) hapo unakuwa salama.
 
Kazi ya Neutral ni nini? Niliamini ndio inatenganisha engine na matairi, lakini baada ya kutafakari na mchoro maelezo naona Ina make sense especially gari zenye shaft ya nyuma. Shaft litaendelea kuzingusha gearbox kutokana na mzunguko wa matairi.
 
Hata gari manual haishauriwi sana kitaalamu kuivuta (towing)
Diff kwa kawaida haipendi mzunguko unaoanzia kwenye matairi.
Ndio sababu trucks kabla ya kuwa towed lazima ukate propeller shaft na uondoe drive shafts (axles )hapo unakuwa salama.
Shukrani, Hii kitu nmeona sana ikifanyika ila sikuwa nafahamu. Nimeongeza kitu.
 
Kazi ya Neutral ni nini? Niliamini ndio inatenganisha engine na matairi, lakini baada ya kutafakari na mchoro maelezo naona Ina make sense especially gari zenye shaft ya nyuma. Shaft litaendelea kuzingusha gearbox kutokana na mzunguko wa matairi.
Ndio maana mwanzoni nilianza kwa kusema nilitamani ningeiganyia video hiyo kitu, kwamaana kwenye video ningezungusha na ungeona kipi kinazunguka na kipi kinabakia stationary.

Sehemu kubwa ya gearbox inazunguka unapovuta gari, sehemu ambazo hazizunguki ni chache sana including hiyo oil pump.
 
Back
Top Bottom