Kwanini wanasema SUPER GRO

Bei yake ni shilingi ngapi nakwanini ukienda kwene maduka ya pembejeo huikuti.? Yn nikama inauzwa kwa connection
Kwasababu super gro sio mbolea na ndio maana Huwezi ikuta kwenyew duka za pembeje
 

Attachments

  • IMG-20221206-WA0006.jpg
    IMG-20221206-WA0006.jpg
    164.7 KB · Views: 30
Mara ya mwisho nilinunua nusu lita kwa 25,000, kuna sehemu wanauza nusu lita 35,000.
 
Wengi mmetema cheche za kutosha ila kila kitu kinahitaji UTAFITI na MAJARIBIO kama hujaitumia super gro kwa kufuta utaratibu ndipo utabaki kusema watu wanaipromo lakini ukishatumia kwa kufuata utaratibu na kuijaribu utaona matokea yake

Kuhusiana na kutokuuzwa kwenye pembejeo ni kulingana mfumo wa biashara wa kampuni inavyosambaza bidhaa zake kwahiyo sio kila kitu kinakua katika mfumo wa biashara uliozoeleka

Kampuni nyingi zinazalisha bidhaa ikiwemo tajwa hapo juu kama gnld kwa upande wangu nasisitizi kua uwe wakala wa hiyo kampuni au usiwe bidhaa yoyote lazima uichunguze na kuijua pia ufanyie majaribio(ikiwezekana) wewe unaweza sema haifai kwa kuhadithiwa na watu ila wenzako waliotumia redhanded wameona manufaa yao

Mimi sidanganyiki. Nimeshawahi kuitumia na sitoitumia tena. Namshukuru Mungu mazingira yangu yanaruhusu kufuga hata kuku kwa kuanzia natumia mbolea ya kuku wangu, na pia msimu wa mvua kukaribia naagiza trip kadhaa za mbolea ya ng'ombe kutoka kwa wafugaji wa ng'ombe. hizo mbolea za dukani nitakuwa nagusisha tu buboost. Nasema hivi kwa sababu kuna mwaka nilipigiwa promo ya Super Gro na mtu ninayemheshimu sana, yaani mbwembwe alizoniwekea nikajisemea mwaka huu patachimbika wakati wa mavuno labda mvua zisumbue. Aisee sijaona tofauti yoyote. Ujinga wa hawa promoters penye kaukweli kidogo wanakujazia sifa kibao. Ni sawa na hawa wanaouza sabuni na mafuta ya kupaka kwenye mabasi.
 
Back
Top Bottom