Kwanini wanaowawekea viongozi sumu hawakamatwi?

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,152
Kwa muda mrefu kumekuwepo taarifa kwamba baadhi ya viongozi wa serikali huwekewa sumu (poison) kwenye vyakula na vinywaji vyao. Ingawa mara nyingine huonekana kama tetesi, ukweli ni kwamba vitendo hivi vimewahi kuripotiwa hata kwa viongozi wakubwa duniani. Mfano ni kiongozi wa Palestina Yasser Arafat aliyefariki mwaka 2004 akidaiwa kuwekewa sumu, Alexei Navalny wa Urusi aliyewahi kushambuliwa kwa sumu mwaka 2020, na rais wa zamani wa Ukraine Viktor Yushchenko aliyenusurika baada ya tukio la aina hiyo mwaka 2004.

Hali kama hiyo pia imeripotiwa nchini Tanzania, hasa katika vipindi vya kisiasa na uchaguzi. Baadhi ya viongozi wamedai kuwekewa sumu lakini wakabaki hai baada ya kupata matibabu kwa siri, kisha baadaye umma ukaja kusikia ukweli. Miongoni mwa waliowahi kutaja tukio kama hilo ni:

  • Mzee Philip Mangula, aliyedai kuwekewa sumu mwaka 2020 baada ya kufanyiwa vipimo vya kitabibu.

  • Hayati Dk. John Pombe Magufuli, ambaye alipokuwa Naibu Waziri aliwahi kusema hadharani kuwa aliwekewa sumu.

  • Paul Makonda, aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na Arusha, naye amedai aliwekewa sumu mwaka jana.
Pamoja na taarifa hizi zote, maswali makubwa bado yanaendelea kuulizwa:

  • Kwa nini wale wanaodaiwa kuhusika na vitendo hivi hawakamatwi wala kufikishwa kwenye vyombo vya sheria?

  • Je, ni kwa sababu ushahidi wa kutosha haupatikani?

  • Au ni kwa sababu kuna mkono wa siri wenye nguvu za kisiasa unaolinda wahusika?

  • Nia kuu ya kuwadhuru viongozi kwa sumu ni ipi – ni ushindani wa kisiasa, kulinda maslahi binafsi, au njama za kupora madaraka?
Hadi sasa, maswali haya yameendelea kubaki bila majibu ya moja kwa moja, jambo linalozidi kuongeza hofu na sintofahamu miongoni mwa wananchi. Ukweli unabaki kuwa, vitendo hivi vinahatarisha maisha ya viongozi na pia vinaweka doa kubwa katika historia ya kisiasa ya taifa.

Pia Soma:
 
Hayo ni matokeo ya kuwa na makundi makundi ndani ya Taasisi moja. Kukamatana ni mtihani
 
Huyo namba Bashite mtoe hapo. Anatafuta tu kiki. Nani wa kumuwekea sumu huyo!
 
Polisi: Mzee Philip Mangula amekutwa na sumu mwilini, ni baada ya kufanyiwa uchunguzi
Umemsahau Dr.Mwakyembe.
 
Muda mwingine watu huwa wanaongea tu kama tetesi ni vitu visivyo na ushahidi,wakati mwingine huwa wanaongea tu majukwaani ili kujisafisha au kupata huruma ya wananchi lkn huwa si kweli
Huyo namba Bashite mtoe hapo. Anatafuta tu kiki. Nani wa kumuwekea sumu hu
 
Wanaokamatwa ni wezi wa kuku tu kibongolendini, wengine wote utasikia tu "wasiojulikana" na hamna cha "mlilo" wala Murilo anataka kuwajua kwa kuwa anawajua!
 
It Better for Ten Guilty Persons to go Free Than that One Innocent Person be Convicted....
 
Inawezekana huwa wanakamatwa lakini hatutangaziwi.
Pia unaweza kumkamata mtekelezaji wa amri, lakini mtoa amri akawa hakamatiki. Wengi wanaoweka sumu wanatumwa tu.
 
Nadhani ni bora tukaacha wapambane na hali yao, je unadhani ni uchungu kiasi gani familia za watu waliopote zinaupitia na hao viongozi hawakutia nguvu kukemea hayo mambo, nadhani ni wakati wa kuwaacha wakajipambanua wenyewe...
 
Back
Top Bottom