Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,709
- 9,030
Ndoa nyingi ni kwa ajili tu ya kulala na kuamka, kulea watoto na kuzeeka pamoja mpaka kifo. Wanandoa wengi ni mara chache sana kupeana busu na kukumbatiana wanapopata habari njema. Mume humuwekea mkewe chakula mdomoni pale tu mke anapokuwa mgonjwa akawa hawezi kujilisha.
Ukimuona mwanaume anamfungulia mlango mkewe basi ujue mlango huo ni mbovu au una kasoro. Kitu pekee kinachomfanya mwanaume wa kiafrika kuigusa shingo ya mkewe ni pale mke huyo anapolalamika kuwa ana homa. Hatoigusa tena mpaka atakapopata homa nyingine. Muda pekee ambao atambeba mkewe mikononi mwake ni pale anapojifungua. Ukiwaona wamekaa nje wakati wa usiku, usifikiri wanaenziana. Wanasubiri tu harufu ya dawa waliyopulizia ndani iishe.
Wanawake wengi wanawanunulia zawadi waume zao pale tu mume anapokuwa mgonjwa hospitalini. Muda pekee ambao wanakimbia pamoja ni pale inapotokea hatari na kila mtu akawa anakimbia. Muda pekee wanaokaa pamoja jioni ni pale wanapotaka kwenda kupeleka malalamiko kwa wazazi wa mtu aliyempiga mtoto wao au aliyempa mimba binti yao.
Muda pekee wanaokoga pamoja ni pale wote wanapochelewa kwenda kazini. Muda pekee ambao mke huyatazama kwa ukaribu macho ya mumewe ni pale jicho la mume linapopatwa na uchafu.
Kwa bahati mbaya, Waafrika wana mawazo kuwa kila mwanaume romantic na mbembezi anakuwa ametawaliwa na mke. Hapo wataanza kueneza umbea. Tubadilike.... Mabadiliko yanaanza na WEWE.