CCM wanamuogopa Lowassa kwa sababu yeye siyo kiongozi wa ndimi mbili!. Alisema jambo analiamini na kulisimamia mpaka mwisho.
Hata hivyo', walimuundia zengwe kumfyeka kisiasa lakini walishindwa, waliogopa kazi wakajiunga kundi, wakafanikiwa kumundoa nchi, hawakuweza tena kuzungumza MKUKUTA, Dira ya Maendeleo2025.
Hata alipoibukia Lowassa ni Mungu na mapenzi ya Watanzania kwake na siyo CCM. Baadhi ya viongozi ndani ya Chama chake wametumia nguvu nyingi Sana kumshughulikia huyu bwana lakini wameumia. Wengine Kama kina Mkama wao badala yake Kama wasisi kauli ambazo hazijakuwa na tija ndani ya Chama wakawa majeruhi Wa kwanza.
Tunapofanya jambo kwa hila lazima tuharibikiwe. Baada ya Watanzania kufuatilia sarakasi za Lowassa na Chama chake, wakagundua ukweli na sasa huruma zao zote ziko kwa huyu bwana.
Hata cha takriban miezi mitatu iliyopita ilipowatuma vijana karibu 30 kwenda mikoa yote kufanya utafiti, juu ya kiongozi gani anayekubalika na wananchi, matokeo yalibainisha ni Lowassa akifuatiwa kwa mbali na Dr. Magufuli.
Huu ndiyo ukweli CCM wanalifahamu na mbingu zinajuwa ukweli huu. Bora tu Watanzania wapewe chaguo Lao tutakuwa tumeepuka mtego tuliojiwekea wenyewe kwa maslahi ya wachache!