Kwanini walioshangilia kujeruhiwa kwa Tundu Lissu hawakukamatwa?

JOESKY

JF-Expert Member
Mar 25, 2015
816
2,032
Katika hizi siku kadhaa za kifo cha magufuli kumeonekana kutokea kwa vitendo kadhaa vya kuonyesha furaha kwa baadhi ya watu na masikitiko kwa baadhi ya watu. Kwa kifupi kumekuwepo na hisia mseto juu ya kifo cha kiongozi Magufuli.

Lakini pamoja na hili kujitokeza tujaribu kurudi nyuma kidogo mwaka ambao Tundu Lisu alipigwa risasi nyingi huko Dodoma eneo la area D makazi ya viongozi wa serikali mchana kweupe na jua kali likiwaka watu wakabeza na kushangilia kwamba Lissu ni msaliti alitakiwa auwawe kabisa.

Katika hali isiyo ya kawaida na ya kusikitisha sana ni kwamba wale wote walioonesha hali ya kufurahi juu ya msiba huu wa Magufulu wamekuwa wakikamatwa na polisi na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria wakati huohuo wale wote waliofurahia Lisu kujeruhiwa wapo huru kukejeli popote pale na wakati wowote ule.

Inasikitisha kuona Tanzania hii chini ya serikali iliyokuwa ya Magufuli kuendeshwa kwa misingi ya uchama yaani polisi badala ya kufuata kanuni na sheria zinasemaje wao wanafanya mambo yao ili kuwafurahisha viongozi wao waliowaweka mamlakani. Ni mara nyingi kama sio mara zote tumeona namna ambavyo hao polisi wakitumika kuwakandamiza wale ambao wanasherehekea msiba wa Magufuli.

Ifike mahali serikali na polisi watambue waziwazi kuwa sherehe za namna hii zina root yake ambayo ni kutoka hukohuko serikalini Mbona alipokufa Mkapa watu hawakusherehekea? Mbona alipokufa Nyerere watu hawakusherehekea? Inakuwaje kifo cha Magufuli kiwaburudishe watu sana mioyoni mwao mpaka kufikia hatua ya kuandaa party kila kona?

Ifike mahali tukubali kuna mahali Magufuli aliteleza katika uongozi wake badala ya kuwaunganisha watu yeye akawagawa na haya ndio matokeo ya hilo pandikizo lake. Kwahiyo wala hata haishangazi kuona watu wakifurahia kifo cha mkuu magufuli hadharani maana ndio roho aliotaka watanzania wawe nayo.

Hatujasahau kauli zote za kina Cyprian Musiba, Paul Makonda, Bashiru Ally, Job Ndugai, Musukuma, na wengine wengi zote hizi zime precipitate kutokea hali tunayoiishi sasa hivi.

Natoa maoni yangu kwa mama Samia Suluhu apambane kwa hali na mali kuhakikisha Tanzania na Watanzania inarudi katika nyakati zile za upendo na mshikamano pasi na kuwa na itikadi za aina yoyote ya kupelekea uvunjivu wa amani miongoni mwetu. Ifike mahali tujifunze kwa kuamini kuwa Kiongozi unatakiwa uwe muunganisha watu sio mtenganisha watu.
 
Kwanza sio uungwana wala ubinadamu kushangilia kifo ama mateso ya mtu mwingine no matter what.

Pili kuna mzungu mmoja aliwahi kutudhihaki kuwa huku Afrika

"all animals are equal, but some are more equal"
 
Kwanza sio uungwana wala ubinadamu kushangilia kifo ama mateso ya mtu mwingine no matter what.

Pili kuna mzungu mmoja aliwahi kutudhihaki kuwa huku afrika
"all animals are equal, but some are more equal"
Huyo ni George Orwell katika kitabu chake cha the animal farm
 
Tumepitia kipindi kigumu sana cha kuoongozwa na mwendawazimu. Ndiyo maana hata mission yake ili bumba big-time.

Still kwa kukataza watu wasimuone Lissu Nairobi Hospital, na kumnyima mshahara na kumnyang'anya ubunge na marupurupu inaacha ushahidi wa Mazingira kuwa Magufuli ndiye mhusika Mkuu wa operation ya kumuua Lissu.

All in All Mungu ameonyesha uwapo kwa Watanzania. Aliyetaka kumuua Lissu amekufa yeye na maiti yake inatembezwa kama biashara ya machinga mitaani
 
Ni upuuzi kutaka kulazimishana furaha, huzuni au kupendwa! Kila mtu aishi maisha yake! Kuwa na huzuni au furaha hutegemeana na aina ya maisha mliyo ishi na marehemu kabla ya kifo chake.

Na jambo hili halipo Tanzania tu! Lipo duniani kote! Leo hii itokee Muizrael akafa, ni kawaida sana kwa Mpalestina kufurahia/kufanya hata sherehe! Sababu ni nini? Ni uonevu tu wa hao Waizrael dhidi ya Wapalestina ndiyo chanzo cha hizo chuki.

Tuishi kwa kupenda kutenda haki! Uonevu, dhuluma, ubinafsi, ubaguzi, ukabila, umungu mtu, ujivuni, ukaidi, nk. Ndiyo chanzo cha baadhi ya watu kufurahia vifo vya wenye mamlaka.
 
Back
Top Bottom