Kwanini walinzi wa getini wakijua unaenda kuomba kazi wanakuwa wakali sana?

Mwonekana wako sometimes nao ni tatizo. Unaenda practical training na ujeuri wa chuoni utafikiri umeajiriwa tayari! Lazima uisome namba
 
Nakumbuka miaka ya ya nyuma nilikuwa mwanachuo kulikuwa na jambo la muhimu sana iatakiwa nionane na katibu mkuu wa wizara fulani... na shida yenyewe ilikuwa lazima nimwambie yeye tu!nilipoenda secretary wake akaniangalia juu chini...nikahisi ntakwama, ubongo ukawa tayari kwa lolote! Akaniambia " Nieleze shida yako au kama ni binafsi nenda nyumbani kwake"! ... nikatabasamu, nikamwambia mie ni ndugu yake amwambie kuwa ndugu yake alie mwambia aje ofisini kwake kaja leo....! Simu ikapigwa.... nikaambiwa niingie! Nilipoingia. ..nikamwambia K.M samahani mie si ndugu yako ni mwanachuo wa chuo fulani...ni na shida kadhaa kadhaa kadhaa... !! KM acheka saana!! Akanisaidia kila nilichohitaji ! Akaniambia siku yoyote niende....akanitoa nje akamwambia secretary. ...mtoto wa dada yangu huyu!!! ..... Nawashauri vijana wa kisasa pia msikatishwe Tamaa na mijitu yenye roho mbaya!
Hapo ulitumia akili sana, hata mm nataka nikamfate magufuli kwa staili hiyohiyo
 
Mi sikwenda kuomba ajira bali nilikwenda kufanya presentation fulani acacia hapo victoria walinzi wa pale wana roho nyeusi utafikiri mkaa. Kuna dada mmoja wenzie wote waliniambia umemkuta huyo dada kauzu.

Walinzi wengi hawajiamini na hawana akili ya kufikiri kwamba office ina internal na external customers.
 
Hata kwenye ulimwengu wa roho wapo hao walinzi wa mageti. Hao wanaokujibu kwa sasa wanatumika tu bila kujijua au kujua. Utakuta mlinzi anakwambia hakuna kazi humu hata kama kazi zipo. Utajikuta unaishia mlangoni tu hata offisin huingii. Vitu vyote vinaanzia ktk ulimwengu wa roho baadaye vinajidhirisha ktk ulimwengu wa kimwili. Wapangue hao kwa kusali na uwafute kabisa. Ili njia iwe clear. Kwa sasa unaweza ona kawaida lakin baadaye utaona kama kuna kitu sasa. Utakuta hata kipindi cha kutafuta kazi yatajirudia kama usipo muomba Mungu sasa. Na kumbuka mlinzi anaweza kuruhusu nan aingie nani asiingie. PRAY
Amen!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom