Kwanini walinzi wa getini wakijua unaenda kuomba kazi wanakuwa wakali sana?

Jitu jeusi

JF-Expert Member
Oct 18, 2015
1,703
2,359
Hivi visa vimenikuta mara nyingi sana, yaani mlinzi anataka umpe bahasha afungue aisome kwanza ili athibitishe kama unaomba kazi au mambo mengine.

1. Leo nimetembelea pale TBC- tazara huu mkasa umenikuta, nilienda kuomba internship ya mambo ya IT.
Mlinzi alinitisha pia akasema watu wa IT ni wezi kwa hiyo mimi naweza iba vitu mule ndani.

2. Issue kama hii ilishatokea Bandarini, pia mlinzi hakutaka niingie ndani hadi nilipozuga naongea na meneja kwenye simu ndo akaniruhusu

Naombeni swaga za kupambana na hawa watu jamani
 
Hata kwenye ulimwengu wa roho wapo hao walinzi wa mageti. Hao wanaokujibu kwa sasa wanatumika tu bila kujijua au kujua. Utakuta mlinzi anakwambia hakuna kazi humu hata kama kazi zipo. Utajikuta unaishia mlangoni tu hata offisin huingii. Vitu vyote vinaanzia ktk ulimwengu wa roho baadaye vinajidhirisha ktk ulimwengu wa kimwili. Wapangue hao kwa kusali na uwafute kabisa. Ili njia iwe clear. Kwa sasa unaweza ona kawaida lakin baadaye utaona kama kuna kitu sasa. Utakuta hata kipindi cha kutafuta kazi yatajirudia kama usipo muomba Mungu sasa. Na kumbuka mlinzi anaweza kuruhusu nan aingie nani asiingie. PRAY
 
Inategemea na ofic,ofic za watu wenye njaa lazma ukutane na wachawi kama hao?
 
Hii Ni kweli, sijui Hawa jamaa huwa wanawaza nini. Sijui wanahisi mtu akiomba kazi anaomba kazi ya ulinzi Kwa hiyo wanabana, wanaboa kweli
 
Hivi visa vimenikuta maranyingi sana, lani mlinzi anataka umpe bahasha afungue aisome kwanza ili adhibitishe kama unaomba kazi au mambo mengine.

1. Leo nimetembelea pale TBC- tazara huu mkasa umenikuta, nilienda kuomba internship ya mambo ya IT.
Mlinzi alinitisha pia akasema watu wa IT ni wezi kwahiyo mm naweza iba vitu mule ndani.

2. Issue kama hii ilishatokea Bandarini, pia mlinzi hakutaka niingie ndani hadi nilipozuga naongea na meneja kwenye simu ndo akani ruhusu

Naombeni swaga za kupambana na hawa watu jamani
Wanajua mkishapata kazi mtawasumbua sana kufungua mageti na magari yenu
 
Nafikiri wote hawako hivyo. Nakumbuka nilienda kutafuta "GREEN PASTURE" kwenye Taasisi moja binafsi.

Wakaniita interview, nikafika pale mlinzi akaniuliza kishikaji tu "UMEITWA KWENYE TAALUMA IPI?" Nikamjibu .... Akanitia moyo kwa kusema tena akitabasamu, "Dah! Mna bahati sana mliosomea taaluma hii. Andika kwenye daftari hili & ukifika mapokezi muulizie HR atakuelekeza."

Sinple tu, wako poa. Inategemea na presentation yako kwao.
 
Hahaha umenikumbusha mbali ilishawahi kunitokea nimeenda kwenye kiwanda cha tbl,mlinzi alinisumbua mpk nikazuga kuwa natafuta field ili tu niingie
 
Hata kwenye ulimwengu wa roho wapo hao walinzi wa mageti. Hao wanaokujibu kwa sasa wanatumika tu bila kujijua au kujua. Utakuta mlinzi anakwambia hakuna kazi humu hata kama kazi zipo. Utajikuta unaishia mlangoni tu hata offisin huingii. Vitu vyote vinaanzia ktk ulimwengu wa roho baadaye vinajidhirisha ktk ulimwengu wa kimwili. Wapangue hao kwa kusali na uwafute kabisa. Ili njia iwe clear. Kwa sasa unaweza ona kawaida lakin baadaye utaona kama kuna kitu sasa. Utakuta hata kipindi cha kutafuta kazi yatajirudia kama usipo muomba Mungu sasa. Na kumbuka mlinzi anaweza kuruhusu nan aingie nani asiingie. PRAY
Kweli bro hapo umenena, nimuhimu tumrudie Mungu kwa nguvu zote kabisa.
 
Nafikiri wote hawako hivyo. Nakumbuka nilienda kutafuta "GREEN PASTURE" kwenye Taasisi moja binafsi.

Wakaniita interview, nikafika pale mlinzi akaniuliza kishikaji tu "UMEITWA KWENYE TAALUMA KIPI?" Nikamjibu .... Akanitia moyo kwa kusema tena akitabasamu, "Dah! Mna bahati sana mliosomea taaluma hii. Andika kwenye daftari hili & ukifika mapokezi muulizie HR atakuelekeza."

Sinple tu, wako poa. Inategemea na presentation yako kwao.
Sio presentation broo, lani anataka kusoma umeandika nn kwenye bahasha, au anakuambia ajaachiwa apointment na boss wake.
 
Tatizo lenu nyie vijana mna nyodo sana....mkifika kwenye banda letu wala hamsalimii kiungwana....badala yake mnaenda moja kwa moja ofisini mkiitwa mnakuja kwa nyodo sana.....

Ndio maana mkituachia vibahasha vyenu tunavichana tu....
 
Similar Discussions

3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom