Kwanini wafanyakazi halmashauri wanaonekana wezi?

stable

JF-Expert Member
Apr 21, 2012
304
439
Wanabodi.

Nimefanikiwa kufanya kazi wizarani (viwanda) nikaona pagumu nikaona niende halmashauri. Nimeona moja ya vitu ambavyo serikali imechemka Ni kuzipa wizara nguvu kubwa sana saana. Kwasababu hiyo influence ya wafanyakazi wa wizara kwa watu wa halmashuri ni kubwa sana na wafanyakazi wengi wa wizara mbali mbali huwatumia wafanyakazi wa halmashuri kama daraja la kutengeneza pesa.

Nini kifanyike.
ufuatiliaji inayofanyika halmashuri iwe chini ya madiwani. Kwakuwa madiwani wananguvu sana huku halmashauri. Pia jambo kubwa ni kuwa serikali iangalie usawa hasa katika kujiendeleza kielimu kwa wafanyakazi wore wizara ma halmashauri watumishi wa halmashauri wengi wananyanyaika sana kwenye swala la elimu.

Ni matumaini yangu viongozi mbali mbali wako humu pia na wasaidizi wa rais. Hili swala liangaliwe kwa mapana.
 
Madiwani ndio wanaogombea tenda za halmashauri..wasipopewa wanatoa maazimio ya afisa wa halmashauri kufukuzwa
 
Madiwani ndio wanaogombea tenda za halmashauri..wasipopewa wanatoa maazimio ya afisa wa halmashauri kufukuzwa

Tatizo la kuwepo kwa "unbalanced relation" kati ya halmashauri na serikali kuu ni pamoja na halmashauri nyingi kushindwa kutekeleza majukumu yao ikiwa ni pamoja na kutegemea zaidi ruzuku kwa zaidi ya 80% hata ktk maisha ya kawaida hizi ruzuku lazima wanaotoa wawe na nguvu zaidi ktk kuzisimamia na kuona zinafanya kazi inavyostahili. pamoja na hili nadhani kuna umuhimu pia wa kutengeneza utaratibu mzuri ktk kupata viongozi kwa maana ya sifa zao nk mfano madiwani zaidi ya asilimia 27% hawajui kusoma na kama wanajua basi hawezi kuandika alichosoma hii ni kazi zaidi ktk kuisimamia halmashauri.
 
nashauri Idara za halmashauri ziwe chini ya wizara husika.Tamisemi haiwezi kabisa imefeli. Watumishi wa halmashuri wananyanyasika sana sana. JPM tusaidie Huku halmashauri wanaofaidi Ni wachache hats sits hawafiki afu ndio wamwhodhi halmashauri nzima. Tofauti Ni wizara..kila mtu Ana nafasi ya kuongeza wlimi. Tena wizaran mtu akienda kusoma watu hufurah kapunguza idadi . Wakatu halmashaur mtu akiwnda kusoma tunajiuliza kwanini kaenda kusoma
 
Kati ya taasisi za umma zenye mchwa wengi na "wachapa kazi" wanaoweza kutafuna gogo zima la mpingo na kulimaliza ndani ya siku moja ni halmashauri.
 
Back
Top Bottom