Nina mifano mitatu kitaani kwetu ya wachungaji hawa wa mifugo jinsi network zao zilivyokata.
Wa Kwanza yeye anaongea peke yake muda wote, wa pili yeye habadili nguo mwwka mzima, wa tatu yeye muda wote anaiwaza Simba club yaani hana stori nyingine zaidi ya Simba na hawa wote wanachunga mifugo ya matajiri wao kwa ujira mdogo sana ila wanaifanya hio kazi kwa moyo kama vile mifugo ni yao yaani hawa feel ile kunyanyasika na kutumika bila malengo na hawana mpango wa kurudi majumbani kwao.
Nilivyohoji watu wakadai hawa wachungaji hulogwa na hao maboss wao wanapoanza kazi huwachanganyia maziwa na mikojo ya punda na dawa nyingine Fulani wanageuka misukule Fulani, sababu nyingine inasemekana kukaa na ng'ombe muda mrefu unapata athari za harufu ya kinyesi chake kwani ng'ombe hula majani mbalimbali mpaka bangi so kale kaharufu kanachanganyika na kinyesi ukikaa naye around muda mrefu ndo inaenda kichwa kinakua kibovu.