Kwanini wachina wapange kulima heka millioni 2.5 DRC za mawese na sio Tanzania yenye amani?

Kwa nini mchina aje badala ya mtu wa Kigoma kufanya??Mnataka aje mchina mmoja kuwaonesha jinsi ya kulima,kuvuna,kukamua,kuchuja na kupack au kuprocess zaidi ...kwa nini wanafunzi kutoka Kigoma wasiende SUA kujifunza kilimo husika?
Ukajifunze wapi wakati kila kitu elimu yote unaipata kwenye smartphone
 
Tanzania ni kwaajili ya uwekezaji mdogo mdogo. Na hasa kama utakuwa na uwezo wa kukwepa kodi. Kama unataka kufuata sheria zote za kodi, kwa sasa, huo mradi haitaweza kukupa faida yoyote.

Kuna rafiki yangu wakati wa kampeni za mwaka 2015, alimchangia Mh sana 50m TZS, alikuwa na matarajio makubwa katika awamu hii. Sasa amenyosha mikono. Ameamua kwenda kuwekeza Burundi. Ameahidiwa mambo mengi ikiwa ni pamoja na usalama. Vitega uchumi vyake vitalindwa na polisi kwa gharama ya serikali.

Dunia nzima kwa sasa wanashindana kuvutia wawekezaji lakini sisi tinajitahidi kufukuza wawekezaji. Na kwenye hilo tutashinda tu maana hatuna mpinzani.
 
Miaka ya 60 Congo ilikuwa ya pili duniani kwa uzalishaji wa Mafuta ya mawese. Machafuko yameifuta haimo hata kwenye kumi bora. Hivi karibuni Kampuni ya kichina ZTE imeibuka wakitaka kuwekeza kulima hekari millioni 2.5 michikichi. Wao hawalengi kutengeneza mafuta ya kula bali 90% ni kutengeneza biodiesel kuwa mbadala wa Petrol na kuuza katika soko la Congo na maeneo jirani. Changamoto kubwa ni usalama kwa wawekejazi hao.

Najiuliza, Kwa nini watu hawa wasitafutwe waje wawekeze huku mapori mengi yamejaa, tuondokane na sarakasi bandari. Tanzania ya Viwanda chini ya Mwijage wale wachina uliowasema kipindi flani kwa nini wasitafutwe na hawa walime angalau hekari laki nne? Kwa nini wanakigoma wasifanye hii kazi ikiwa ni aibu kuleta muwekezaji kuzalisha mafuta ya mawese wakati wapo watu wenye uwezo wa ufanya hayo japo kwa hekari Laki moja?



najiuliza na kuwaza, maana nilikuwa nadhani mafuta haya huwa yanatoka humuhumu nchini kabla ya sakata hili la mafuta ya kula kuibuka. Siku zote najua ni mafuta ya Pamba kutoka kanda ya ziwa.

mitale na midimu
nawaza kializeti lkn natafakari kimafuta ya kula yenye rehemu
Walime juu ya jiwe lenye laana haitaota
 
Kwa nini mchina aje badala ya mtu wa Kigoma kufanya??Mnataka aje mchina mmoja kuwaonesha jinsi ya kulima,kuvuna,kukamua,kuchuja na kupack au kuprocess zaidi ...kwa nini wanafunzi kutoka Kigoma wasiende SUA kujifunza kilimo husika?
Rubbish unafikir tunazungumzia kilimo cha kijijin kwenu kolomije?Akili gani mfu hizi za kishirikina
 
Kwa nini mchina aje badala ya mtu wa Kigoma kufanya??Mnataka aje mchina mmoja kuwaonesha jinsi ya kulima,kuvuna,kukamua,kuchuja na kupack au kuprocess zaidi ...kwa nini wanafunzi kutoka Kigoma wasiende SUA kujifunza kilimo husika?
Viwandaaaaaaa
 
Siasa za hii nchi ni za level nyingine mkuu hata wakija hao wachina watapigwa zengwe tu..nadhani unatufahamu sisi watanganyika kindaki ndaki kwa kutokupenda maendeleo yeyote...
 
Wanachofuata ni zaidi ya mafuta ya mawese, DRC ni zaidi ya shamba la bibi, kuanzia Rwanda mpaka Belgium wanaitafuna. Jiwe kakataa huo upuuzi.
 
Kule shamba la bibi watapata zaidi ya kile kilichowapeleka.
1 Watakata misitu na hawaichomi wala kulaza chini ioze, wataisafirisha ikiwa magogo kwenda China. Ulizia Indonesia.
2. Wakianza kulima mawese wafanyakazi wa ndani wote na baadhi ya vibarua watatoka China.
3. Kule maporini kuna wanyama wa kila aina. Nyoka kitoweo chao kikuu, wanyama wengine wa nyama kama swala na digidigi hata viboko watafaidi hawanunui nyama ng'o.
4. Tembo watakoma! Watapeleka meno yoote yanayopatikana karibu na kwenye msitu ule.
5. Watajigawa makundi hawa wanalima wengine wanachimba. Watatafuta mpaka dini la mwisho maana wanajua DRC kuna kila aina ya madini.
6. Mkongo asitegemee kupata mafuta pale. Wese litapelekwa likiwa lilivyo ili wapate wese, mbegu yake ikamuliwe itoe mafuta kama yale ya nazi lakini haya first class, ngozi watatengenezea karatasi na nyingine wataibadilisha iwe mbolea kwa ajili ya mashamba yao huko China.

At the end of the day mKongo atabaki na mbuga iliyoserereka bila hata mti, wanyama wataisha, ardhi itaharibiwa, umaskini kwa wakongo utazidi na Kabila atatawala mpaka kifo maana ana kila silaha ya kumlinda. Amen

Msiombee miradi ya wageni ya wese ije nchini. Jifunze far East mjue wanavyolia.
Watu wanadhani wachina wamefuata kilimo cha mawese, wapewe hekari 2.5mil si watavuna kila kilichomo ndani ya hilo eneo!

Congo ni zaidi ya shamba la bibi, kila aingiaye huvuna, misitu imekuwa mali halali ya Rwanda, madini yamekuwa mali ya Wazungu wakiongozwa na Belgium na France, wachina pia wanabeba copper utadhani ya kwao.

JK aliuza gesi yote, leo hii tunaanza kufikiria jinsi ya kupata umeme wa bei nafuu coz ile gesi haina faida kwetu, tunalipa trillions of shillings ili kulipa uwekezaji wa gesi ambao kwetu sio tija tena.

Hakuna mtu mweupe anaekuja Africa kijinga, wote ni wanyonyaji tu.
 
Kulima DRC ni sawa kwasababu wanaopigana wengine wataajiriwa katika mashamba. Nchi ya amani watatuuzia mafuta kwasababu pesa ipo, haijaisha katika vita.
 
Kumbe nina kazi ya ziada ya kupigana vita ya ushindi ya KUJITEGEMEA kwanza kifikra na kisha kihali zote. Hata hivyo lazima ushindi upatikane.
---
Mleta Uzi kanishtua.
 
Ungesoma maana ya thrd, usingekuja na mchango wa kizembe kama huu. Ushabiki wa kuzomea Yanga au Simba kwa kila jambo, unauhamishia JF. Kwa nini husomi mawazo ya wenzako na angalau ujifunze?
Hofa kioja yako kwangu mwisho Lumumba
 
Back
Top Bottom