PreGE2025 Kwanini wabunge wasikatwe posho zao kusaidia huduma za afya?

PreGE2025 Kwanini wabunge wasikatwe posho zao kusaidia huduma za afya?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Wont be the same

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2024
Posts
1,564
Reaction score
2,483
Mchambuzi Skawa Jr. amehoji baada ya Mbunge wa Iramba Mashariki, Francis Mtinga, akichangia Mjadala wa bajeti ya Wizara ya Afya jana Juni 2, 2025 kuomba Watanzania kukatwa kiasi cha Tsh 100 kwenye kila vocha ya 1000 atakayonunua ili kuchangia huduma za afya.
 
Yaaan kila jambo mwananchi akatwe, tumekosa kabisa fikra, mbinu, ubunifu za kutafuta vyanzo vya fedha, huku tukiwa na mapori tele, mito, mabwawa, maziwa, bahari. Hapo hujagusia ufugaji
 
Hapo ndo utaona madudu yaliyopo kwenye utawala husika.

Ikiwa mbunge kila kikao anakula hela ya posho. Hela ambayo mwananchi anaeambiwa akatwe anaitafuta mwezi mzima au zaidi bila kuipata ile hela ...
Wachilia mbali ruzuku na mishahara yao minono..

Ikiwa nchi ina huruma na wanyonge wanaowatawala haitaweza kutafakari kabisa kwa mnyonge anaehaha njaa hela yake kwenda kuimega.

Na badili yale wao kwa wao walipaswa kukatwa kulingana na mishahara yao.
 
Back
Top Bottom