Kwanini wabunge wachukizwe na MwanaHalisi?

ungonella wa ukweli

JF-Expert Member
Mar 27, 2012
4,210
555
Waku habari zenu,

Nimesikia kwenye kipindi cha Tuöngee Asubuhi, kwenye jicho letu ndani ya habari, mtangazaji kasema kuwa baadhi ya wabunge wamewatisha wahusika waliolifungia gazeti la mwanahalisi kutolifungulia, vinginevyo watadili nao wakingilifungulia watawatambua! Je tatizo ni nini? Je wabunge hao wanafaa kuendelea kuwawakilisha watanzania?

Naomba tutoe maoni yetu juu ya hili.
 
Alisema ni wabunge gani? Kama hawezi kubainisha(thibitisha) afute kauli yake!!!
 
Mwanahalisi ulikuwa ni msumali wa moto ! Wabunge wenye tabia za ufisadi , rushwa , wizi na magumashi mengine ,hatutegemei walipende hilo gazeti , bali ungetutendea haki kama ukiwaweka wazi ili tuwaorodheshe kwenye lile daftari letu la Maadui wa nchi.
 
Hufuatilii media wewe ZITTO, ndo alisema hakuna kuwa rafiki wa KUBEBENWA.
Kubenea sio Gazeti la Mwanahalisi. Kubenea ni Kubenea tuu,na gazeti la Mwanahalisi litabaki kuwa Mwanahalisi kwa vile lina sera zake hata kama zinafanana na tabia binafsi za Kubenea.
Usizunguke mbuyu,kama Zitto alimwambia yule bwana(kama ni kweli)usiwe rafiki na Kubenea haimaanishi kuwa asiwe na mahusiano na Mwanahalisi ambalo limesajiliwa kisheria na lina watendaji wengi wenye fikra tofauti tofauti.
 
wakilibania mwanahalisi tutaanzisha jingine linaloitwa chamoto hilo ndo balaaa mbona watafurahi we ngoja tu
 
Mwanahalisi liliwahi kuandika habari ya kiuchunguzi inayoonesha uhusiano na mawasiliano ya siri kati ya Zitto na Mkurugenzi wa usalama wa taifa ambao kwa afya ya CHADEMA ulikuwa si mzuri. Katika hali hiyo si dhani kama Zitto atapenda gazeti hilo lifunguliwe kwa sababu lilishaanika baadhi ya siri zake
 
Halikuwa likiandika habari za kujenga taifa bali kuchochea chuki na migogoro katika jamii
 
Hao wabunge lazima watakua ni wale mafisadi maana MWANAHALISI ilikua mwiba kwa mafisadi.
 
Halikuwa likiandika habari za kujenga taifa bali kuchochea chuki na migogoro katika jamii


Jina unalotumia, comments ulizotoa na makala zilizokua zinatolewa na Mwanahalisi, napata shida kuamini kama ulikua msomaji mzuri wa gazeti hilo.
 
Tumelikosa MwanaHalis mda mrefu sasa lakini kuna mtu mmoja aliniambia laweza funguliwa any time...
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom