Ndugu wanaJF, nimekuwa nikifuatilia bunge kwa karibu sana na nimeweza kubaini haya.
1. Wabunge wa CCM wanawaonea wivu wabunge wanaoikosoa bajeti ya serikali na hviyo kwa vile wao wanaogopa kufanya hivyo, wanaonesha kukerwa na michango inayoikosoa bajeti ya serikali ili iboreshwe vizuri zaidi.
2. Wabunge wa CCM wanageuka wasemaji wa serikali kuliko kuisadia serikali iwajibike na kuwatumikia wananchi vizuri zaidi.
3. Wanaunga mkono hoja asilimia 100 hata kama ina kasoro za msingi. Kwa vile wabunge wa CCM ni wengi zaidi na kwa vile iwe na kasoro au isiwe nazo, bejeti itapita tu. Ni mara chache sana wanaweza kusababisha bajeti ifanyiwe marekebisho na kuboreshwa.
4. Kama serikali imeleta bajeti bungeni ili ijadiliwe - kujadili maana yake ni kusema yale mazuri na mabaya na kupendekeza namna ya kuiboresha.
5. Badala ya wabunge wa CCM kuchangia bajeti wao wanapoteza muda wao mwingi kuanza kukosoa na kuhariri michango ya wabunge wasio wa CCM. Je, ni kweli wanajua maana ya kujadili?