Kwanini waafrika wachache sana wamechukua tuzo ya Noble?

Talented Land

Senior Member
Feb 4, 2016
157
135
Habari za saa hii
Nimekuwa nikifuatilia tuzo za noble kwangu mimi ninaziona kama tuzo zenye heshima kuliko zote katika nyanja za sayansi ,biashara na uchumi bila kusahau amani
Nirudi katika pointi yangu kwa nini waafrika hawachukui hii tuzo?
Fizikia kuna tuzo moja tu toka mwaka 1901(Algeria)
Kemia kuna tuzo tatu(2 misri 1algeria)
Je watu weusi tuna nini hatushindi sayansi tunapewa tu za amani kama
Mandela
Dosmond tutu
Mkenya mama mathai
Na wole sonyika ya literature
Je kuna ubaguzi maana wamarekani 300+ mkenya1 ,ghana1
Je afrika hatuko interest na hizi tuzo?
 
jaribu kuapply mkuu, anza wewe ili baadaye ulete mrejesho
 
Mkuu waafrika tuko nyuma katika nyanja za sayansi, biashara na uchumi hivyo hatukidhi vigezo vya kupata tuzo hiyo.
Katika nyanja za sayansi wanapewa watu waliogundua mambo mbalimbali ya kisayansi na yaliyohakikishwa (approved) kisayansi mfano Ugunduzi wa dawa/chanjo ya magonjwa. Biashara na uchumi pia hutolewa kwa wasomi na wachumi walioweza kutatua migogoro ya kiuchumi. Sisi hivi vitu tunakosa na ndio maana hatupati hizo tuzo.

Kwa upande wa amani afrika ndio inaongoza kwa machafuko, kuna uroho wa madaraka, watawala wengi hawataki kutii katiba za nchi zao hususani inapokuja suala la mihula ya uongozi, wengi wamekuwa wakibadilisha katiba ili waweze kutawala muda mrefu mf Kagame, Nkrunzinza,Mugabe, Kabila , hayati Gaddafi, Museveni nk......

Afrika inakosa vigezo vingi kama suala la utawala Bora, demokrasia, hivi vyote vinatufanya kukosa tuzo za Nobel.
Afrika ukosefu wa demokrasia na ukosefu wa utawala Bora, haya upelekea migogoro, rushwa iliyokithiri, ufisadi, wizi wa mali ya umma nk.....

Katika suala la utunzaji wa mazingira bado tupo nyuma sana hivyo tunakosa vingezo katika kila nyanja na ndio maana hatupati tuzo za Nobel.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom