maramia
JF-Expert Member
- Jul 17, 2015
- 2,030
- 1,345
Sakata la upungufu wa sukari limenisukuma nijiulize swali moja muhimu, kwamba kuna sababu gani za msingi na za kisayansi zilizopelekea viwanda vyote vya Kagera, Mtibwa, Kilombero na TPC Moshi vifungwe kwa wakati mmoja na kusababisha upungufu mkubwa wa bidhaa hii adimu? Na kwanini visiachiane muda kufunga uzalishaji?
Pamoja na hilo, kwa upande wangu naona kama kuna mahusiano ya kihujuma kati ya viwanda hivi vya sukari ambavyo vinamilikiwa na wahindi na wasambazaji wa sukari nchini ambao katika sekeseke hili la ufichaji sukari imeonekana karibu wote ni waasia.
Ebu waziri mwenye dhamana na jambo hili au mwingine yeyote anayewajua wamiliki wa viwanda hivi na wafanyabiashara wenye leseni za kusambaza sukari atuwekee hapa ni akina nani ili tutafakari mahusiano yao.