Uchaguzi 2020 Kwanini Viti Maalum Bungeni?

Mkandara

Verified Member
Mar 3, 2006
15,536
2,000
Yawezekana kuna upotoshaji wa makusudi kabisa juu ya uwepowa viti maalum bungeni kuwa ni nafasi wanazopewa vyama vya Siasa kuchagua Wanawake wa vyama hivyo kuingia Bungeni kama Wawakilishi wa vyama husika. Nadhani swala hili linahitaji kujadiliwa Upya na Elimu itolewe kwa Wananchi na wahusika.

Sheria zinazotoa Mwongozo kuhusu viti maalum ni pamoja na:-- Katiba; Sheria ya Taifa Ya Uchaguzi; na
Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2010 hivyo ni muhimu sana Wananchi wote kuzingatia kwa nini uwepo wa viti maalum Bungeni.

Imeelezwa bayana kuwa: - Viti maalum ni viti vilivyotengwa kwa mujibu wa sheria kuhakikisha kwamba watu au makundi ya watu wenye mahitaji maalum na ambao si rahisi kugombea Uchaguzi na kushinda kwa sababu ya hali yao (kama ulemavu na Uchache wao) wanapata nafasi ya kuwakilisha maoni na vipaumbele vyao katika ngazi tofauti za Uongozi (Bungeni, Wilayani, Halmashauri).

Kwa mujibu wa Sheria hizi, haya makundi yaloainishwa mpaka sasa katika bunge letu ni WANAWAKE na WALEMAVU. Na kwa upande wa Wanawake, Vyama vya Siasa vimepewa nafasi ya KUPENDEKEZA majina ya Wagombea wa Viti Maalum na sii KUTEUA majina hayo lengo likiwa hawa ni Wawakilisha wa shauri na maoni ya WANAWAKE WOTE nchini katika mahitaji yao dhidi ya Mfumo Dume ambao awali maamuzi yote ya Kijamii yalifanywa na Wanaume bila kushauriwa na Wanawake. Na Hapa ndipo Upotoshaji wa viongozi wa kisasa unapotokana..

Hivyo basi, Wabunge wa viti maalum iwe WALEMAVU au WANAWAKE ni Wawakilishi wa makundi yao na sii Vyama vyao bali Chama kinapendeleza tu majina ya Wawakilishi na vema zaidi ifahamike pia viti Maalum vimewekwa kama sehemu ya kuvutia Wanawake kushiriki katika Siasa za nchi yetu (Affirmative action) na ndio maana hupitishwa Wanawake wa viti Maalum 1/3 ya Bunge letu.

Sasa inapotokea mvutano baina ya Vyama na Wawakilishi wa Wanawake aidha wamependekezwa na Chama cha Siasa au Laa, nadhani ipo haja kubwa sana ya kufanya marekebisho ya Katiba na Sheria hizi ili kuwapa WANAWAKE mamlaka zaidi ya kufanya Maamuzi wao badala ya kutegemea Vyama vya Siasa. Aidha vyama vya Wanawake vifanye uchaguzi wao au wateuane wao wenyewe kupitia Mabaraza yao na sii vinginevyo.

Tumesikia mengi bunge la 11 kuhusu unyanyasaji wa Wanawake ndani ya vyama vya Siasa. Viti maalum vikitumika kama rushwa na biashara ya Ngono na kadhalika, udhalilishaji wa Wanawake umefikia hatua ya viongozi kusahau hata malengo yake kwa jina la Vyama vya Siasa. Bila shaka tumefika wakati Wanawake nchini kuwa kitu kimoja kwa maslahi yao maana safari yao wote ni moja.

Walisema TUKIWEZESHWA TUNAWEZA sasa iweje leo nafasi za Viti Maalum ziwe kigezo kikubwa cha malumbano ya Kisiasa? Nashauri Kuundwa Chombo kimoja cha UMOJA wa WANAWAKE kupitisha majina ya Wawakilishi wao badala ya Uongozi wa Vyama ambao bado mfumo Dume umetamalaki.
 

antimatter

JF-Expert Member
Feb 26, 2017
8,062
2,000
....Viti maalum ni viti vilivyotengwa kwa mujibu wa sheria kuhakikisha kwamba watu au makundi ya watu wenye mahitaji maalum na ambao si rahisi kugombea Uchaguzi na kushinda kwa sababu ya hali yao (kama ulemavu na Uchache wao) wanapata nafasi ya kuwakilisha maoni na vipaumbele vyao katika ngazi tofauti za Uongozi (Bungeni, Wilayani, Halmashauri).
Halima Mdee, Esta Matiko, E. Bulaya, Nusrat Hanje,.... hawana uwezo wa kugombea na kushinda?!!!
 

Odhiambo cairo

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
14,614
2,000
Tatizo tulilonalo Tanzania ni tume ya uchaguzi kutokuwa huru . Mengine yanawezekana, ikiwa ni pamoja na wanawake kuzigombea badala ya kusubiri uteuzi wa vyama.

Tume imedhibitiwa na watawala. Hivyo hata upatikanaji wa wanawake hao imejaa Siri. Kama ilivyotokea safari hii.
 

Mkandara

Verified Member
Mar 3, 2006
15,536
2,000
Halima Mdee, Esta Matiko, E. Bulaya, Nusrat Hanje,.... hawana uwezo wa kugombea na kushinda?!!!
Hoja yangu ni kuwapa nafasi Wanawake watakao simamia na kutetea haki zao pamoja na kushiriki kikamilifu katika Utungaji Sheria na usimamizi wa Serikali haijalishi kina nani, majina yao ama nafasi zao ktk vyama. Kinachotakiwa hapa ni Wanawake wajichague wenyewe na sii kuingiliwa na Wanaume..
 

Bungua

JF-Expert Member
Jul 28, 2018
927
1,000
Yawezekana kuna upotoshaji wa makusudi kabisa juu ya uwepowa viti maalum bungeni kuwa ni nafasi wanazopewa vyama vya Siasa kuchagua Wanawake wa vyama hivyo kuingia Bungeni kama Wawakilishi wa vyama husika. Nadhani swala hili linahitaji kujadiliwa Upya na Elimu itolewe kwa Wananchi na wahusika....
Upuuzi hauwezi kujengewa hoja! Umeshindwa kwa viwango vyote. Si kila anayekupigia makofi anakushangilia.
 

mhanila1

JF-Expert Member
Dec 15, 2017
1,018
2,000
Kama kungekuwa na nia ya dhati ya kupanua demokrasia na kuondoa huo unyanyasaji ambao kinara wa kwanza ni chama tawala wangeruhusu wagombea binafsi hapo kungekuwa hakuna shida chama kikimfukuza mbunge anabakia kama mbunge binafsi na hata hivyo viti wa wabunge maalum visingekuwa tatizo.

Lakini kwakuwa nia ya chama tawala ni kuwakalia kooni wabunge wake waendelee kutegemea chama pekee cha kuwateua ndiyo maana kunakuwa na mawazo ya kuonewa. Chakushangaza unasikia watu wanasema CHADEMA inanyanyasa wanawake lakini ndiyo chama pekee kilichokiwa na wagombea wa ubunge wanawake 62 idadi ambayo vyama vingine vyote wakijumlishwa wagombea wao wanawake hawafikii 62.

Wagombea hao wengi walienguliwa na tume ya uchaguzi kuonesha kwamba bado NEC wanaendekeza mfumo duma kwakuwa wanawaona wanawake hawawezi kuwa na Sifa za kuwa wabunge wa majimbo. Hili ni tatizo kubwa katika nchi yetu.

Ni vema hao wabunge wa viti maalum wakaachiwa walemabu wengine kama hao wanawake wakahamasishwa kugombea katika majimbo kama walivyo kuwa wameanza CHADEMA na vyama vingine vingeweza kufanya hivyo kuongeza idadi ya wabunge wanawake wanaogombea katika majimbo na kuondokana na mambo ya viti maalum ambavyo ni vya makundi yasiyoweza kugombea majimboni.

Hivi kweli hadi leo kuna mwanamke ambaye anaona yeye hawezi kugombea jimboni, tuache kuwadharau wanawake tuwahamasishe wagombee kwenye majimbo na hayo mambo ya viti maalum vibakie kwa ajiri ya walemabu tu.

Tu ruhusa wagombea binafsi ili kuondoa tatizo la vyama kufukuza wabunge wakuchaguliwa katika vyama vyao na kutusababishia garama za uchaguzi bila sababu ya msingi. Kufanya hivyo kutatatua mambo mengi ikiwa ni pamoja na baadhi ya viongozi kiwatambia wanachama wao kuwa kama wasiposifia hawatawapisha kugombea ubunge na kulazimika kuomba mapambia usiku na mchana.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom