Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 52,669
- 119,297
Wanabodi,
Huu ni uzi wa swali tuu,
"Kwanini Viongozi Wetu Wanaogopa Sana Mabango Hadi Kuwadhibiti Washika Bango Kama Wahalifu?!. Lengo la mabango yote duniani ni kufikisha ujumbe, sasa mabango yanahatari gani hadi yaogopwe namna hii?!.
Tanzania ni nchi yetu sote, nikimaani ni malí ya sisi Watanzania wote, japo miongoni mwetu wako wenyenchi, walanchi na wananchi, hivyo kunapotokea matukio ya machukizo kwa jamii kama jinsi yule mama wa jana alivyodhibitiwa.
Kwa mujibu wa sheria mkusanyiko usio halali (unlawful assembly) lazima uwahusishe watu zaidi ya watatu, yule mama alikuwa peke yake na amenyanyua tuu juu bango lake, wanausalama walikuwa na sababu gani ya kumdhibiti kama mhalifu? .
Hata kama lengo la udhibiti ule ni kumzuia asije kuleta madhara kwa rais, mtu yuko mmoja tuu peke yake, tena mwanamke, bango lake amelishika kwa mikono miwili, angeleta vipi madhara au hilo bango ndio limegeuka silaha hatarishi?!.
Kuna ubaya gani kama viongozi wakisoma mabango yoyote ya kuwafikishia ujumbe wowote?!. Kwa nini viongozi wetu wanaogopa sana mabango? .
Asante sana na pongezi kwa rais wetu Mhe. John Pombe Joseph Magufuli kumnusuru yule mama na kuupokea ujumbe wake, hivyo huo ni mwanzo mzuri, na ikibidi awaruhusu tuu wale jamaa waandamane nchi nzima na wafanye mikutano yao usiku na mchana kwa amani na utulivu ili mpate fursa ya kuyasoma hayo mabango yao kwa makini maana mengine yana ujumbe kuntu, kutatokea madhara gani kama watu wakiachwa waandamane tuu watakavyo, na kuhudhuria mikutano watakavyo? .
Kufuatia tukio la jana, nashauri kuanzia sasa kikosi chá ulinzi chá viongozi akiwemo rais, kijumuishe walinzi wa kike ili kuzuia udhalilishaji wa kijinsia kama tulioushuhudia jana kwenye ile mubashara.
Na baada ya njia ya kushika bango ku proove kuwa very successful kufikisha ujumbe, kuanzia sasa tutegemee mabango mengi mengi kwenye kila ziara za viongozi, hivyo natoa wito kwa viongozi wetu, tutendeeni haki bila kusubiria mabango, na hata Chadema na wana Ukawa, hakuna tena haja za kuomba vibali vya maandamano, mambo yote sasa ni kwa mabango tuu na ujumbe utafika!.
Nawatakia Furahi Dei Njema
Paskali.