Kwanini Viongozi wetu hawajamtumia vyema Will Smith katika kutangaza utalii wetu.

Jan 20, 2014
32
49
Hivi karibuni kumekuwa na urushwaji wa picha za mchekeshaji na muigizaji maarufu wa kimarekani aitwae Will Smith akiwa katika mbuga zetu za wanyama lakini cha ajabu wala sijaona taasisi husika ama wizara wakitumia nafasi hiyo kufanya naye matangazo kuijulisha dunia ujio wake katika mbuga zetu za wanyama..
a94516a96be6c4af976cb8e8db217b9e.jpg
 
Hizi wizara zimajaa watu walio kosa ubunifu na huenda hata hawajui will smith ni nani.
 
Ziara zingine ni private,mteja hataki usumbu,hataki kutanga\wa na hataki interview amekuja kupumzika utafanya nini hapo.
Walioko Arusha kwenye sekta ya utalii wanalifahamu hilo.
Kuna watu maarufu na matajiri wengi sana wanakuja kimya kimya,lakini ndio hivyo vigezo na masharti huzingatiwa.
Abromovich alikuja na wasaidizi 100,hakutaka chochote zaidi ya kupumzika,sasa kama mtu kaja na watu 100 mnahangaika kumuhoji wa nini tena
 
Sio kumhoji ila kuhakikisha wanatumia media zingine kutangaza ujio wake nimuhimu mno sio lazima wafanye naye matangazo ila kupitia picha zake wanaweza kuzitumia vyema mbona kapiga picha na maguides...
 
We unategemea hao FAFAFAFAFAFA wawe na mtazamo wa kuitangaza nchi yetu? lahasha itachukua karne nyingi sana hao watu kuelewa umuhimu wa utalii wao wanachokijua pekee ni kutuongezea kodi kila mwaka badala ya kutumia rasilimali tulizonazo kutuingizia kipato cha kutosha angekuwa Uhuru kenyatta Hapo angeshaitumia hiyo fursa siku nyingi sana
 
Sio kumhoji ila kuhakikisha wanatumia media zingine kutangaza ujio wake nimuhimu mno sio lazima wafanye naye matangazo ila kupitia picha zake wanaweza kuzitumia vyema mbona kapiga picha na maguides...
wanakuwa na masharti sana.Huwezi kumtumia tajiiri akufanyie matangazo,inategemea na brand na class,na wengi wao wanakuja wana pesa ndefu wanakuja kutulia tu hawataki vurugu.
Patrick Kluivert anashusha sana wachezaji wenzake wa zamani,lakini hawataki kujulikana.
HAWATAKI KUTUMIWA,WAMEKUJA KUSTAREHE.
 
Oooh poa kaka... nimeona mipicha online nikaona baadhi ya media kama ya uganda wamepost online kwamba Will Smith Katua Uganda ndo nikajiuliza kwann sisi hatuitumii nafasi hiyo.
 
Usitusumbue tunakagua kwanza vyeti..........angekuwa jakaya angemwita ikulu
 
Oooh poa kaka... nimeona mipicha online nikaona baadhi ya media kama ya uganda wamepost online kwamba Will Smith Katua Uganda ndo nikajiuliza kwann sisi hatuitumii nafasi hiyo.
WaTz wako usingizini TTB, NCAA, na tanapa wanasubiri trip za mbele wanakuambia wanaenda kutangaza utalii! Habari kama hizi tu hata kuziweka kny media zinawashinda! Uko sahihi, siyo lazima kufanya nao interview ndio tupublish uwepo wao...
 
Back
Top Bottom