Kwanini "vijidrama" viwaumize watu?

Kwanini "vijidrama" viwaumize watu?

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2023
Posts
7,645
Reaction score
10,867
Tanzania ni nchi ya amani! Haiwezi kuwa na matukio ya utekaji!

Neno la "mkubwa" ni kama "Sheria". Imeshatamkwa kwamba kinachoitwa utekaji nchini ni "vijidrama" tu.

Ndiyo maana Sativa "alipojiteka" na kujipiga risasi, Polisi hawakuwa na cha kufanya. Hawashughuliki na vijidrama!

Deusdedith Soka naye "alijiteka" na kutokomea kusikojulikana mpaka sasa. Polisi wako kimya kwa kuwa ni "vijidrama"

Marehemu Ally Kibao alijiteka, akajitesa hadi kufa! Hata hivyo Polisi hawawajibiki kwa lo lote kwa kuwa ni vijidrama!

Hivi karibuni, Deogratius Tarimo naye alifanya jaribio la "kujiteka" akishirikiana na "washkaji" wake, na baadaye akaenda kukaripoti hako "kadrama" kake kituo cha Polisi. Ingawa picha za "alioshirikiana" nao zimeonekana mtandaoni, Polisi hawatajisumbua na "vijidrama" kama hivyo.

Kwa jinsi tulivyofundishwa shuleni, drama hulenga kuburudisha na kuelimisha!

Kwa nini "vijidrama" viumize, vitese, viue na kusababisha simanzi?

PIA SOMA
- Kuelekea 2025 - Napinga Kauli ya Rais Samia kwamba Utekaji ni Drama, hii ni dharau kwa Wananchi
 
Vijidrama vinavyotokana na kuahirisha kufikiri kizalendo, a.k.a kujizima data
 
Huyu maza ile kauli ni kama aliitoa kama hakufikiria kauli yake ina impact gani negative. Hebu fikiria katibu wa ccm katwangwa risasi huko iringa . Lakini watu wanalichukulia kama drama mtandaoni.. Dah!
 
Back
Top Bottom