Mara nyingi tumesikia matangazo mbalimbali yakihamasisha jambo fulani, mwisho mwa Tangazo utasikia vigezo na masharti kuzingatiwa. Ni kwa nini hivyo vigezo na masharti visisemwe ili kama mtu utaamua kushiriki na ukishindwa kusiwe na sababu?
"Vigezo na masharti" ni janjajanja iliyofichwa utakayokutana nayo baadae baada ya kuwa umeshacommit. Mfano mdogo ni say ticket ya ndege. Wanaweza kukutangazia kwamba bei ni as low as $90. Ukiingia king tu, unakutana na VAT, sijui ma levy gani, aiport tax, IATA tax, na makorokoro kibao. Mwisho wa siku unajikuta umelipa $200. Hivyo ndo vigezo na masharti boss.
Mara nyingi tumesikia matangazo mbalimbali yakihamasisha jambo fulani, mwisho mwa Tangazo utasikia vigezo na masharti kuzingatiwa. Ni kwa nini hivyo vigezo na masharti visisemwe ili kama mtu utaamua kushiriki na ukishindwa kusiwe na sababu?
unapoisikiliza vizuri tangazo la bidhaa ndani ya yale maelezo kuna kitu unaambiwa kufanya ukienda kinyume hujafata yale maelekezo it means hujakidhi vigezo,
mf: tangazo moja la mtandao wa simu... tangazo linanadi.... ili uingie kwenye droo lazima ununue kifurushi cha intaneti kuanzia 1000 na kuendelea kwenye menu mpya... vigezo na masharti kuzingatiwa/ Sasa ukijiunga kifurushi chini ya 1000 hujazingatia kigezo, pia ununue kifurushi cha 1000 cha intaneti kwenye menu ya zamani it means hujakidhi vigezo.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.