Kwanini utawala unaogopa upinzani kuliko wakati mwingine wowote katika historia

fazili

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
13,819
18,553
Hakuna aliyejua kwa uhakika kama Trump angekuwa rais wa 45 wa Marekani lakini ndio hivyo amekuwa.
Watu walifikiri David Cameroon angemaliza muda wake kama waziri mkuu wa Uingereza, yalitokea ya kutokea kutoka kusikotarajiwa hakumaliza
Kuna yumkini nyingi mno katika siasa na sasa hasa katika ulimwengu huu wa sasa ambako wanadamu wanapata taarifa kwa haraka, kwa undani na kwa usahihi zaidi kuliko siku za nyuma
Hii inawapa uwezo watu kuamua kwa haraka mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kubadilisha misimamo na mitizamo yao
Mabadiliko siku hizi ni kama jadi na hakuna anayeweza kujua nini kinafuata kwa mwanadamu ambaye ndiye MWAMUZI wa mambo hatabiriki tena siku hizi
Watawala wanalijua hili na linawatia hofu kubwa, chochote chaweza kutokea kwani WAPINZANI walishafikisha hadi 40% ya kura zote pamoja na MBINU zote za watawala na kuifanya serikali iliyopo kuwa iliyochaguliwa na watu wachache zaidi katika historia yetu (54% ya kura zote). Na hapo ni baada ya MBINU kubwa sana kutumika. Kwa hiyo HOFU ni kubwa sana kwani haijulikani nini kitatokea siku zijazo.
 
Ndo maana Biblia inasema ...kila kitu kwa kiasi.. Kiongozi anapaswa kubalance mambo. Geji isiegemee upande mmoja. JK alisemwa na JPM anasemwa kwa kushindwa kwao kuwa na kiasi..
 
Tatizo ni kwamba upinzani ukifikia stage wakianza zungumzia incompetency za jamaa itakua shida kwa jamaa maana staili iliyomuingiza madarakani hata yeye anajua....ni....
 
Hakuna aliyejua kwa uhakika kama Trump angekuwa rais wa 45 wa Marekani lakini ndio hivyo amekuwa.
Watu walifikiri David Cameroon angemaliza muda wake kama waziri mkuu wa Uingereza, yalitokea ya kutokea kutoka kusikotarajiwa hakumaliza
Kuna yumkini nyingi mno katika siasa na sasa hasa katika ulimwengu huu wa sasa ambako wanadamu wanapata taarifa kwa haraka, kwa undani na kwa usahihi zaidi kuliko siku za nyuma
Hii inawapa uwezo watu kuamua kwa haraka mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kubadilisha misimamo na mitizamo yao
Mabadiliko siku hizi ni kama jadi na hakuna anayeweza kujua nini kinafuata kwa mwanadamu ambaye ndiye MWAMUZI wa mambo hatabiriki tena siku hizi
Watawala wanalijua hili na linawatia hofu kubwa, chochote chaweza kutokea kwani WAPINZANI walishafikisha hadi 40% ya kura zote pamoja na MBINU zote za watawala na kuifanya serikali iliyopo kuwa iliyochaguliwa na watu wachache zaidi katika historia yetu (54% ya kura zote). Na hapo ni baada ya MBINU kubwa sana kutumika. Kwa hiyo HOFU ni kubwa sana kwani haijulikani nini kitatokea siku zijazo.
hata mi nashangaa ...upinzani wa sasa hv unapinga kila kitu kuliko wakati wowote katika historia
 
Back
Top Bottom