Mtama kwa watoto
JF-Expert Member
- Mar 31, 2014
- 394
- 150
Habari zenu wana MMU.
Sikuzote napenda kuchangia lakini leo limenikaa kwenye Roho naomba niliseme yalojiri.
Wifi yangu amekuja kwetu yeye watoto wake na shoga yake kwa ajili ya likizo mpaka 12jan 14.
Huyu shoga wa wifi yangu namshangaa nyumba ina watoto wa kiume mumewangu anavaa KANGA moja
mara kaingia chumba cha watoto wa kiume,yani tangu aje ni 10days lakini nimeshamshibaa.
Jumamosi kaenda Disco karudi saa mbili asubuhi yaani amepita sitting room nguo alovaa Aibu nimeona mie.
Sasa leo asubuhi nimeamka kutengezeza chai ya Mzee namkuta kalala sitting room kihasara pembeni kuna Condom.
Nikaenda kumfata wifi yangu akamuamshe, wakati naenda kazini vijana ndani wanasema hawaendi Chuo sababu wanaumwa, sasa sijui zile condom zimetumiwa nanani na yaani amekosa adabu anafanya hayo mambo kwenye sofa jamani hivi nikimwambia wifi yangu shoga yako aondoke nitakua nimekosea?
Uzuri kuwa mume wangu aliuliza kwanini huyu binti amekuja muda mdogo hapa lakini kengele kila mara? mie sikujibu wifi akasema ah kaka siunajua tena friends.
Waungwana mwenzenu hata sijui nifanyeje zaidi linalo nikera lile la kuvaa kanga moja anamanisha nini?
hahahhahaa acha wivu wewe, acha kabisa aisee ngoja vijana wafaidiMamaye zake....
Timua haraka sana....
Tena fungasha virago tupa nje...
hahahhahaa acha wivu wewe, acha kabisa aisee ngoja vijana wafaidi
....Waungwana mwenzenu hata sijui nifanyeje zaidi linalo nikera lile la kuvaa kanga moja anamanisha nini?
Yaani wifi,mitoto yake na shoga yake firauni wanajazana kwangu.....
Kwanza tuwaulize walikuwa na vero la mchele...
Khaaa kuna watu wanyonyaji sana...
Huyo wifi si mzuri....
Mie ningeanza na wifi kwanza au kamletea kakake mwanamke?
Weeeeee...Waungwana mwenzenu hata sijui nifanyeje zaidi linalo nikera lile la kuvaa kanga moja anamanisha nini?
Habari zenu wana MMU.
Sikuzote napenda kuchangia lakini leo limenikaa kwenye Roho naomba niliseme yalojiri.
Wifi yangu amekuja kwetu yeye watoto wake na shoga yake kwa ajili ya likizo mpaka 12jan 14.
Huyu shoga wa wifi yangu namshangaa nyumba ina watoto wa kiume mumewangu anavaa KANGA moja
mara kaingia chumba cha watoto wa kiume,yani tangu aje ni 10days lakini nimeshamshibaa.
Jumamosi kaenda Disco karudi saa mbili asubuhi yaani amepita sitting room nguo alovaa Aibu nimeona mie.
Sasa leo asubuhi nimeamka kutengezeza chai ya Mzee namkuta kalala sitting room kihasara pembeni kuna Condom.
Nikaenda kumfata wifi yangu akamuamshe, wakati naenda kazini vijana ndani wanasema hawaendi Chuo sababu wanaumwa, sasa sijui zile condom zimetumiwa nanani na yaani amekosa adabu anafanya hayo mambo kwenye sofa jamani hivi nikimwambia wifi yangu shoga yako aondoke nitakua nimekosea?
Uzuri kuwa mume wangu aliuliza kwanini huyu binti amekuja muda mdogo hapa lakini kengele kila mara? mie sikujibu wifi akasema ah kaka siunajua tena friends.
Waungwana mwenzenu hata sijui nifanyeje zaidi linalo nikera lile la kuvaa kanga moja anamanisha nini?
Yaani wifi,mitoto yake na shoga yake firauni wanajazana kwangu.....
Kwanza tuwaulize walikuwa na vero la mchele...
Khaaa kuna watu wanyonyaji sana...
Huyo wifi si mzuri....
Mie ningeanza na wifi kwanza au kamletea kakake mwanamke?
Hakuja hata na pini, Na zaidi asivyo kua na haya yeye ana watoto wa4 watoto hawasikii Juzi kuna mmoja amekula Mpaka ametapika, mtoto ameshakula na wenzie 1 na nusu usiku wamecheza Saa 3 wakunywa maziwa na wenzie halafu kulala ndio routine kwangu, huyu mtoto asione mtu anakula anataka mtoto Hata kama kulala anamuamsha...
Huyo shoga wa wifio asie na maadili ningekuwa mimi siku tatu tu zingetosha kumfangashia mizigo yake
Fukuza wote. Kwanza uyo wifi yako si mwema kwako. Chunguza kuna kitu iweje aje na rafiki yake mwezi mzma.
Then rafiki mwenyewe kicheche asije kukupindua mana awa mawifi nao sazingine ni balaa.
Nyumbani kwangu kabisa!Ningekuwa mimi hata ushauri nisingekuja kutafuta huku,name hizo Sikh kumi zingekuwa nyingi sana kwa yeye kuendelea kuwepo........
Nasubiri wanaume watupie neno,ni kwa jinsi gani wamelichukulia.