Kwanini ukishaoa ndugu wa w/wake huamia kwako?

Kwanini ukishaoa ndugu wa w/wake huamia kwako?

stata mzuka

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2012
Posts
4,834
Reaction score
1,765
Wakubwa shikamoon,wamakamo zangu mambo vp na wadogo zangu hamjambo?
Nimefanya research moja hivi nimeona ktk jamii yetu inayotuzunguka m/ume akishaoa tu basi mwaka hauishi m/mke japo sio wote utaona anachachukua wadogo zake wawili anakaa nao haijalishi nyumba ni ya kupanga au yenu bila kuangalia kipato chako na pia na pia huchukia ndugu wa m/ume wakikaa hapo nyumban,,nasema hivyo sio kwamba sipendi ndugu la hasha bali naona km mtu ndo kwanza unaanza maisha bado hujajipanga then hapohapo unaletewa mtu tena wa kumsomesha kabisa nafikir ndo sababu mojawapo ya kutoendelea vzuri...
Natangaliza samahan kwa yeyote nitakayemkwaza na uzi huu,,Nawasilisha
 
Hilo tatizo vinginevyo kama mume umeridhia kupata mtu wa kusaidia hapa na pale
 
ah mie nadhani hayo mambo watu wanamuwa hawajaongelea kabla ya kuoana.
alafu ukumbuke wengi wetu tunajikuta inabidi uwazsaidie wadogo zetu
 
Mmh, huko ulipofanyia research tu ndo wana tabia mbaya. Sie kwetu kiutamaduni, ndugu wa mwanamke hawakai kwakeakishaolewa.

Ila nikuulize, kwako uwezo ni nini? Kama umekuta mwanamke anasupport wadogo zake kuwasomesha etc, unaona nongwa gani kuishi nao? Mbona mamako anaweza kuja kuishi na wewe bila kujali kama nyumba mmepanga ama la?
 
Hilo tatizo vinginevyo kama mume umeridhia kupata mtu wa kusaidia hapa na pale
Utakuta mwingine hajaridhia bali anajilazimisha kwani mwisho wa cku huwez kumwambia aondoke kwako
 
Hii inachangiwa mashemeji kutafunwa na baba mwenye nyumba anafidia mahaari aliyo toa.
 
Kwaupande wangu sioni mbaya aje baada ya mwaka,na pia sio eti namtegemea mumewangu ndio anisomeshee mdogo wangu nafanya kazi yeye wala hatoi pesa yake na matumizi ya nyumbani tunasaidiana na istoshe yeye ndio anapata
sifa wala sio mie..
 
Mmh, huko ulipofanyia research tu ndo wana tabia mbaya. Sie kwetu kiutamaduni, ndugu wa mwanamke hawakai kwakeakishaolewa.<br />
<br />
Ila nikuulize, kwako uwezo ni nini? Kama umekuta mwanamke anasupport wadogo zake kuwasomesha etc, unaona nongwa gani kuishi nao? Mbona mamako anaweza kuja kuishi na wewe bila kujali kama nyumba mmepanga ama la?
Mkuu ukisoma uzi wangu vzuri utaelewa,,na maanisha hapo m/ume ndo anakuwa kila kitu ktk familia bdo hajamuwezesha mke wake
 
this is serious issue and very true. why mke hujifikiria wao zaid?si wote ila ni aslilimia kubwa
 
Sidhani kama hiyo ni RESEARCH kama ulivyoiita bali umeweka kile ulichokishuhudia mahali
 
ah mie nadhani hayo mambo watu wanamuwa hawajaongelea kabla ya kuoana.
alafu ukumbuke wengi wetu tunajikuta inabidi uwazsaidie wadogo zetu

Kusaidia hatukatai ni bora utoe msaada wakiwa nyumban kuliko ile kuhamia kabisa then hujajipanga mi na mfano m1 hapa mtaan kwetu jamaa kaoa na mtoto m1 akiishi ktk 1single room mdogo wa mkewe alikuja kumsaidia dada ake ktk kipindi yu mzaz lkm mpaka sasa hiv hajarud kwao na yupo anakaa ktk chumba cha jirani kwn hawez lala chumba kimoja basi jamaa alimwambia mke wake amuambie mdg wake arudi nyumban mke anashindwa kumwambia na jamaa pia anashindwa kumwambia shemej yake
 
Hii inachangiwa mashemeji kutafunwa na baba mwenye nyumba anafidia mahaari aliyo toa.
Hahahah u make me lough mkuu
 
stata mzuka... nafikiri kupata suluhu ya tatizo hili ni wewe kuzungumza na mwenzi wako.
Na mazungumzo haya yataeleweka na yatazaa matunda kama kipato chako au niseme chenu kiko wazi, na namna mnavyotumia pia iko wazi (transparency is key).

Kama unamwambia mkeo hali ngumu anaelewa.. kwa hyo hao ndugu wasio na ulazima hutawaona... Na kama msaada wa shule ni wa lazima sn, basi wanaweza kuupata wakiwa kwa wazazi hivyo kupunguza garama za mahitaji mengine wakiwa kwako.
 
Last edited by a moderator:

Ni kwel mkuu you right kabisa nafikiri tatzo letu kubwa ni kutokuwa wa wazi
 
Last edited by a moderator:
Ok hilo ni sawa.watu wengi wanasahau kuongea mambo mengi kabla ya kuingia kwenye ndoa.
 
Ukisema research unakuwa umejibana sana mkuu, nina imani research ina-involve sample kubwa zaidi. Hujaona nyumba nyingine wageni waliojaa ni wa mume na wala si mke? Mimi nafikiri uamuzi unabaki wa wanandoa, kama wana uezo wa kuhudumia hao wageni wao au la, manake kuwakwepa haiwezekani. Ila wageni na wenyeji wote wanatakiwa kupima upepo ukoje jamani, sasa watu wana chumba kimoja mgeni na wewe umo tu!
 
Haina shida kwani ndivyo tulivyolelewa kutegemeana na kutoana kimaisha...sidhani kama hao ndugu huja bila makubaliano na mume/mke kuridhia pia...sina hakika na tafiti yako!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom