ZeMarcopolo
Platinum Member
- May 11, 2008
- 14,279
- 7,681
Katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu 2015 ushirikiano wa vyama wa UKAWA utashindwa vibaya. Hali hii ni bayana kwa wale wote wanaofuatilia hali ya kisiasa tangu CCM ilipomchagua mgombea wake mpaka hivi sasa.
Sababu kubwa itakayowafanya UKAWA washindwe vibaya ni kubalika kwa mgombe wa CCM Dk. John Pombe Magufuli na mikakati madhubuti ya CCM kuusaka ushindi. Hata hivyo kuna sababu nyingine mbili za ndani ya UKAWA wenyewe zitakazochangia kuwaangusa:
1. Kushindwa kutoa ujumbe unaoeleweka
2. Kushindwa kuratibu shughuli za kampeni na mahusiano ndani ya UKAWA.
Katika kufutilia Kwangu mijadala mbalimbali nimeona kuwa wanoitetea UKAWA hawana ujumbe zaidi ya kusema lengo lao ni kuitoa CCM. Kauli hii ni sawa na kusema lengo lao ni kupata madaraka tu. Kuingia madarakani bila kuwa na mkakati ni ujumbe unaoweza kukubaliwa na wafuasi kindakindaki ambao wala huna haja ya kuwaomba kura. Unapoenda kumuomba kura mtu asiye mfuasi wako ni lazima uwe na ujumbe zaidi ya kutaka madaraka. Hili litaiangusha sana UKAWA kwenye uchaguzi huu.
Kwenye kushindwa kuratibu shughuli za uchaguzi na mahusiano ndani ya UKAWA imedhihirika kuwa kila kukicha kunaibuka mgogoro mpya. Watu walioajiriwa na kampeni hawapati malipo, mgawanyo wa majimbo na kata hauheshimiwi na hakuna mkakati mmoja wa kutafuta ushindi.
Katika uratibu, kuna kosa kubwa sana la kiufundi ambalo UKAWA wanalifanya. Kuna majimbo mengi ambayo wagombea wa UKAWA zaidi ya mmoja wamerudisha fomu. Katika majimbo hayo yapo ambayo wagombea wengine wameamua kutokufanya kampeni na kumuachia mwenzao, lakini yapo pia ambayo wagombea zaidi ya mmoja wanafanya kampeni. Kutokanana sheria y uchaguzi, wagombea wote waliorudisha fomu majina yao yatakuwepo kwenye karatasi za kura. Hii itasababisha kura nyingi za wagombea wa UKAWA kuharibika na kugawanyika. Uchaguzi wa mwaka huu unaweza kuwa na kura nyingi zilizoharibika kuliko chaguzi zote katika historia ya nchi yetu.
Tafiti mbaimbali zinaonyesha watu wengi (zaidi ya asilima 40) wanategemea kuona UKAWA kwenye karatasi ya kura. Hata hivyo tafiti hizo hazielezei watu hao baada ya kutoona UKAWA, wale ambao lengo lao lilikuwa kuchagua UKAWA watafanyaje. Kwa kiasi kikubwa watu wa namna hii wataharibu kura kwa kuchagua mtu zaidi ya mmoja na wengine kuchagua wa chama chao hata kama siye aliyeachiwa nafasi ya UKAWA.
Kushindwa kwa UKAWA kwenye uchaguzi wa mwaka huu kunatokana na maandalizi hafifu na kuendeshwa na matukio. Hili ni fundisho kwa chaguzi zijazo...