Kwanini Uendelee Kuteseka na Msongo wa Mawazo?

Kwanini Uendelee Kuteseka na Msongo wa Mawazo?

Konzo Ikweta

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2013
Posts
766
Reaction score
1,535
Kwa mujibu wa Dr.Karl Albrecht kupitia kitabu chake cha “Stress and Manager”(1979) anasema kuna aina nne za “Stress” ambazo mtu hukutana nazo kila siku.

AINA YA KWANZA: TIME STRESS (Stress inayotokana na Muda).

Stress hii hutokea pale ambapo unaanza kuhisi hauna muda wa kutosha kufanya majukumu yanayokukabili *(Mambo mengi ila muda mchache)*. Utaanza kuisikia pale ambapo unakuwa na *“deadline”* ya kitu na bado haujaikamilisha,umechelewa kufika mahali (mf: Kuchelewa usafiri, ofisini, kwenye kikao n.k).

Stress ya namna hii inaweza kukupelekea akili yako kukwama kufanya kazi, kuanza kujiona hauwezi tena kupata suluhisho, inakuingizia hofu, inakufanya ukate tamaa na inakupelekea kukosa raha kabisa.

UFANYE NINI???

i/. Jifunze kuweka orodha ya majukumu yako kila siku *(To do list):* Usianze siku kwa kukimbizana na kila kitu. Andika chini kwanza mambo yote muhimu unayotakiwa kuyafanya siku hiyo na yafuate. Usipokuwa na orodha utakuwa “Unadonoadonoa” kila kitu kama kuku.

ii/. WekaVipaumbele *(Prioritization):* Kumbuka kila jukumu lina uzito tofauti. Baada ya kuwa na orodha ya siku, Jiulize: Ni mambo gani muhimu zaidi? Hakikisha haufanyi yasiyo ya muhimu zaidi kabla HAUJAMALIZA yaliyo ya MUHIMU.

iii/. Jifunze Kusema Hapana *(Learn to say No):* Kuna watu wengi sana wanaiingia kwenye stress kwa sababu ya kujiingiza kwenye kila kitu kinachokuja. Wanataka wahusike kila kikao,waonekane kila mahali, wamridhishe kila mtu hadi mwisho wa siku wanajikuta wamekubali kufanya mambo mengi kuliko muda walio nao.Kusema HAPANA sio UKATILI bali ni KUWAJALI wengine ili USIWAANGUSHE kwa kuwapa matumaini usiyoweza kutimiza.

Je,umeshawahi kukutana na stress hii ya kwanza?Njia gani utaanza kuitumia leo kati ya hizi tatu?Tukutane kesho tuendelee.

#Nanauka
IMG-20190613-WA0069.jpeg
 
Back
Top Bottom