Kwanini tuvuti nyingi za Tanzania zipo kwenye lugha ya kingereza

kazz

Member
Sep 13, 2012
24
7
wadau na ombeni msada wenu nashwindwa kuelewa kwa nini tuvuti nyingi za Tanzania zikiwemo za serekali na watu binafsi zinachapishwa kwa kingereza huku walengwa tukiwa ni raia wakawaida kabisa ambao wengi wetu hatuko vizuri na hiyo lugha

hilo lakwanza jambo jingine nathani hili linakera kuliko hilo lakwanza nimauthui ambayo yapo kwenye hizo tuvuti.

ngoja nitoe mf utakuta shirika, kampuni au taasisi inadai kwamba inafanya shughuli flani labda uendelezaji wa software lakini Zaidi ya ukurasa mmoja ambao ni broncher ambayo inaoyesha taasisi ambazo wanafanyanazo kazi hakuna taarifa zozote zile ambazo zina ushawishi wakutosha kwamba wao wanafanya hiyo kazi na wanaifahamu "technically"

kufupisha kitaalamu ilitakiwa kuwe kuna sehemu yakublog hapo walitakiwa wawe wanaelimisha katika kile ambacho wanakifanya hii ingesaidia kujenga
Uaminifu kati ya mpokeaji huduma na mtoa huduma
Lakini zaidi yahapo hayo ambayo wanakua
Wanafundisha kama unataka kutumia usemi huo
Yatakuwa naathari kubwa sana katika jamii
Nabinafsi sioni chochote kile watakacho poteza
Zaidi ya kuwa wazalendo kwenye jamii ambayo
Wanaihudumia.

Ningependa nihitimishe kwa kusemema
Fani ya teknologia imekuwa kwavile watu wame share na wanaendelea kushare ufahamuu wao
Kwa kasi hata kama umtu ameumia vipi
Kujua jambo flani lakini baada yakulijua
Ameshare ule utaalamu wake kitu ambacho
Kimekua nifursa siyo kwake tu bali na engine

Kwa kweli hapa tunabidi tubadilike tena kwa kasi haijalishi uko kwenye sector gani lakinini kushare mambo yenye tija ni minimum
Nathani kama kuna marketing strategy zuri ni hii.

Kwanini hatuifuati hapo ndipo napo hitaji mchango wako unathani kwamba shida iko wapi?
 
Ujue lugha rasmi nchini mwetu ni mbili, kiswahili na kiingereza. Nionavyo mimi tovuti za kitaaluma kuchapisha taarifa zake kwa kiingereza ni sawa tu kwa kuwa lugha ya mawasiliano kwa wasomi kuanzia kidato cha kwanza shuleni hadi vyuoni ni kiingereza.

Na English ni lugha ya kimataifa. Afu kwenye computer kiingereza ni rahisi kuliko kiswahili.

Sasa kama wanatangaza habari zinazohusu wananchi wetu tu kwa kiingereza hapo solution ni kwenda english kozi tu!
 
Ujue lugha rasmi nchini mwetu ni mbili, kiswahili na kiingereza. Nionavyo mimi tovuti za kitaaluma kuchapisha taarifa zake kwa kiingereza ni sawa tu kwa kuwa lugha ya mawasiliano kwa wasomi kuanzia kidato cha kwanza shuleni hadi vyuoni ni kiingereza. Na English ni lugha ya kimataifa...
Kuna contradiction kwenye swala la lugha, lugha ya kiswahili ni lugha ya taifa nandiyo tunayo itumia lugha ya kingereza wanasema ni bussines language hapo ni siyasa.

lakini hata kama by default tuseme tunaongea kingereza which is not true bado hizo tuvuti kwenye sector ya uelimishaji ziko nyuma sana kwa sababu ukipita kwenye hizo site zetu pamoja nakwamba hizo broncher zao zimechapishwa kingereza lakini ku pata knowledge siyo rahisi kwa sababu hicho kipengele ketu hakipo regardless ya lugha iliyo tumika kufikisha ujumbe
 
Kuna contradiction kwenye swala la lugha, lugha ya kiswahili ni lugha ya taifa nandiyo tunayo itumia lugha ya kingereza wanasema ni bussines language hapo ni siyasa.

lakini hata kama by default tuseme tunaongea kingereza which is not true bado hizo tuvuti kwenye sector ya uelimishaji ziko nyuma sana kwa sababu ukipita kwenye hizo site zetu pamoja nakwamba hizo broncher zao zimechapishwa kingereza lakini ku pata knowledge siyo rahisi kwa sababu hicho kipengele ketu hakipo regardless ya lugha iliyo tumika kufikisha ujumbe

Apa walikosea kusemaga lugha ya taifa ni kiswahili ndugu mahakamni tuh sheria kibao ni english
 
Katika ulimwengu wa biashara inaweza kuwa sawa kutegemeana na kundi la wateja wanaolengwa haswa.

Yaani kuna wateje wanao takiwa sana ila kuna wale waje wasije ni sawa tu..

Hivyo mtu anapoandaa website yake anafanya akiwa na picha ya aina ya wateja anaowalenga haswa.

It's all about business and marketing.
 
Katika ulimwengu wa biashara inaweza kuwa sawa kutegemeana na kundi la wateja wanaolengwa haswa.

Yaani kuna wateje wanao takiwa sana ila kuna wale waje wasije ni sawa tu..

Hivyo mtu anapoandaa website yake anafanya akiwa na picha ya aina ya wateja anaowalenga haswa.

It's all about business and marketing.
Ndiyo hilo unalosema ni sahii lakini kwenye site za serekali na mashirika ya umaa sithani kama wao wako sahihi kuwa wanatumia kingereza hiyo haijakaa sawa kwa namna yoyote ile. Alafu licha ya lugha ya kingereza kua inatumika bado mauthui yenye kuelimisha ambayo jamii ingeweza kunufaika nayo iwe ni kwa kiswahili au kingereza bado hakuna.
 
website biashara inayotoa huduma hapa Tanzania kuwa na lugha ya kingereza nikupoteza hela tu, ndio maana website nyingi na vingereza vyao huwa zipo ilimradi kampuni ionekane ina website.
Website ni chombo cha kuvutia wateja, sasa kama hauzungumzi lugha yao utawakosa hao wateja.

Unapoandika kingereza maana yake umelenga watu ambao hawajui kiswahili, sasa jiulize Tanzania ni wangapi ambao hawajui kiswahili?

maoni yangu Tovuti zinazotoa huduma hapa Tanzania ziwe kwa lugha ya Kiswahili alafu unatengeneza tovuti mfanano ya pili kwa lugha ya kingereza(kama ukipenda).

Pili, kama mleta mada alivyo sema kublog ni muhimu ilikuelimisha wateja, na kwa lugha ya kiswahili ndio inafaa zaidi kwasababu unauhakika asilimia kubwa atakaye soma anafahamu lugha.

Wageni wenyewe ambao hawajui kiswahili wanapambana sana kujifunza kiswahili, mimi naona hakuna haja ya kuandika kingereza kama biashara yako inatoa huduma hapa Tanzania.
 
Back
Top Bottom