Kwanini tutumbue majipu gizani?

Kibo10

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
11,277
8,850
Wakati nachambua wagombea Urais niliwahi kusema "pamoja na sifa nyingi nzuri alizo nazo mgombea wa CCM, JPM - Anao udhaifu mkubwa sana kwenye eneo la kusimamia Uwazi, Utawala Bora, Demokrasia na Haki za Binadamu".

Kitendo cha serikali kulizuia Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) lisirushe matangazo ya Bunge moja kwa moja "LIVE" ni dalili nyingine tosha kuwa serikali ya sasa inao mpango kabambe wa kujiendesha kwa siri huku ikiogopa kuhojiwa.

Kama serikali imejipanga kutumbua majipu na ilishaanza kazi hiyo tena ikiifanye mbele ya KAMERA, inaogopa nini wananchi wakiwaangalia wawakilishi wao moja kwa moja?

Na kama bunge letu litakubali kuendesha vikao vyake kwa "SIRI" bila wananchi kuona LIVE litakuwa bunge KIBOGOYO kuliko yote yaliyowahi kupita na hata huyu rafiki yangu JOB NDUGAI ntamdharau kabisa.

Hoja ya rafiki yangu Nape Moses Nnauye ati uamuzi huo umefikiwa ili kubana bajeti ni ya kitoto mno, hata mtoto wa chekechea hawezi kudanganyishiwa!

Kama serikali haina gharama mbona AZAM, ITV na wengine wanataka kurusha matangazo hayo LIVE kwa gharama zao? Mbona serikali haiwaruhusu! Na kama inapunguza matumizi kwa nini ISIFUTE MBIO ZA MWENGE?

Kama JPM mwenyewe pia anaafikiana na uamuzi huu basi nchi itapita kwenye janga!

Mtatiro J.
 
Very sad, sijui Tanzania inaelekea wapi. Naona mikono ya viongozi wetu ipo busy kuivuranga nchi yetu. naona Mungu pekee ndo atatunusuru, kwa sababu wana wa giza wanazidi kuwa na maguvu dhidi ya watoto wa nuru.
 
Tatizo mabadiliko aliyoyahubiri magufuli watu hatukuyaelewa, kiukweli haya ndo mabadiliko, haijalishi tunasonga mbele au tunarudi nyuma ila ni mabadiliko!
 
Back
Top Bottom