Kwanini tusiwe na ujenzi shirikishi?

Kwanini tusiwe na ujenzi shirikishi?

getrusa

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2013
Posts
2,150
Reaction score
1,824
Wakuu habari za majukumu. Nimewaza kidogo kwanini tusiwe na ujenzi shirikishi katika miradi ya barabara..?
enzi zile kabla ye enzi hizi wanakijiji walikuwa wanajitolea kutengeneza ama kuchonga barabara za vijiji na mitaa yao kwa kutimia majembe.! Na kuwa na uhakika kuwa barabara zile zingepitika majira yote ya mwaka.!
katika zama zetu hizi za leo kwanini hawa wakandarasi wasipewe kazi ya kusimamia ubora tu lakini ujenzi wa hizo barabara usihusishe serikali za kijiji na mitaaa na wananchi wenyewe?

Kwa kufanya hivi natumai kwanza tungeweza kuwa na uangalizi wa karibu wa barabara zetu kwani inaowahusu ndio walioitengeneza.

Pili tutatengeneza ajira kwa wananchi wengi walio vijijini na pesa itarudi katika mzunguko wa maeneo husika.!

Tatu kurithisha taaluma ya ujenzi kwa vijana katika namna halisia pale watakapokuwa wakielekezwa namna ya kuifanya barabara kuwa imara kwa maeneo korofi..

Tano jamii kuona imethaminiwa na kupewa hadhi inayostahili ya ulinzi wa miundo mbinu inayoizunguka hivyo kuepusha uwizi na ufisadi sabbu wao wenyewe ndio watakao kuwa wanufaika wa miradi hiyo..!

Mwisho namna hii ya miradi ya barabara ipo katika Nchi za Malawi na Msumbiji..
pamoja na kuwa Malawi ni Nchi Maskini lakini barabara na miundo mbinu yake ni bora na salama sabbu wananchi maskini wameshirikishwa na kuelezwa umuhimu wake kwao.!

Naomba kuwakilisha.
 
Back
Top Bottom