Kwanini Tundu Lissu hafai kuwa Mwenyekiti wa TLS? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini Tundu Lissu hafai kuwa Mwenyekiti wa TLS?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Dr.Godbless, Feb 17, 2017.

 1. Dr.Godbless

  Dr.Godbless JF-Expert Member

  #1
  Feb 17, 2017
  Joined: Sep 28, 2010
  Messages: 713
  Likes Received: 289
  Trophy Points: 80
  Habari wadau,

  Kwa takribani wiki sasa kumekuwa na mjadala mkali juu ya Mgombea wa Uenyekiti wa TLS Mhe. /Mwanaharakati /Wakili Mahiri Tundu Antipas Lissu.

  Nimaamini Kamati ya Uchaguzi ya TLS, kwa kuwa inaundwa na mawakili wote, Na katiba yao wanaifahamu kwa undani zaidi wamezingatia vigezo vyote vya kisiasa, kisheria na kimaadili kupitisha jina la Tundu Lissu, Na kwamba Lissu anakidhi sifa na Vigezo vya kuwa Mwenyekiti wao, wao Mawakili.

  Hivyo basi ni jukumu Lao wenye chama kuamua matakwa yao bila ushawishi wa taasisi yeyote ya Nje.

  Mjadala ulioanzishwa juu ya kumkataa Lissu umejengwa katika dhana ya Hofu, Uchama na Ukandamizaji wa taasisi zenye weledi katika kuhakikisha sheria za Nchi zinalindwa.

  Hoja ya Mwakyembe kwamba Wajumbe wawe makini na kumchagua Lissu, Na kwamba anaweza kuifuta taasisi, sio tu ni kinyume cha sheria bali ni maelekezo mahsusi kwa Wagombea tofauti na Lissu, kwamba Serikali inawapigia kampeni Wagombea wengine kwa kigezo cha kukifuta chama.

  Kwa kifupi Lissu anafaa, Na mawakili wanaoona nyakati, Na matakwa ya Nchi kwa sasa wanajua nini cha kufanya. Niwatakie Uchaguzi mwema. It's time to draw a bold line.

  To go for Mwakyembe au To go for National Interest.
   
 2. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #2
  Feb 17, 2017
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 8,695
  Likes Received: 1,844
  Trophy Points: 280
  Wanasheria wa Tanzania wamelala mno .......... sasa ni wakati muafaka kupata Kiongozi atayewaamsha!! Wakipoteza hii nafasi basi itachukua muda mrefu sana kurudisha heshima yao!!

  Wanasheria gani hao wanapelekeshwa kama Walimu ....................!!
   
 3. K

  Kihava JF-Expert Member

  #3
  Feb 17, 2017
  Joined: May 23, 2016
  Messages: 916
  Likes Received: 676
  Trophy Points: 180
  Nitawadharau na kuwashangaa hao mawakili/wanasheria ambao siku zote wanaitwa wasomi kama hawatamchagua msomi Tundu Lissu halafu eti wafuate ushauri wa 'mwakiembe', sijui 'mwakipapai"!
   
 4. kmbwembwe

  kmbwembwe JF-Expert Member

  #4
  Feb 17, 2017
  Joined: Aug 16, 2012
  Messages: 6,234
  Likes Received: 1,245
  Trophy Points: 280
  hafai huyo big mouth ndio mwanzo wa tls kufutwa mkimchagua. atageuza tls chama kwenye ukawa. simnaona ukawa sasa ni chadema peke yake?
   
 5. georgemwaipungu

  georgemwaipungu JF-Expert Member

  #5
  Feb 17, 2017
  Joined: Jul 7, 2015
  Messages: 2,739
  Likes Received: 337
  Trophy Points: 180
  Shida ni weledi wa Lisu unawatia kiwewe ila ni zamu ya Lisu.
  Maaana kwenye katiba watuburuza mpaka wanaona aibu kuileta ili tuipigie kula maana wanajua tutaikataa
   
 6. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #6
  Feb 17, 2017
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,372
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  Lissu ni mweledi sana ....
   
 7. Dr.Godbless

  Dr.Godbless JF-Expert Member

  #7
  Feb 17, 2017
  Joined: Sep 28, 2010
  Messages: 713
  Likes Received: 289
  Trophy Points: 80
  Kwa hiyo Waliompitisha Walikosea?? Kwamba Mwakyembe na wewe mko sahihi kabisa.?If that's the case nahisi Mawakili wataoneka wamekosea kwa matakwa yako na Gov, ila wenye chama wanatafuta mtu sahihi katika nyakati sahihi. Mawakili watanyakua fursa ambayo ni kumpata Lissu
   
 8. Dr.Godbless

  Dr.Godbless JF-Expert Member

  #8
  Feb 17, 2017
  Joined: Sep 28, 2010
  Messages: 713
  Likes Received: 289
  Trophy Points: 80
  Lissu ni fursa. Mawakili wasipoitumia sasa ni juu yao.
   
 9. E

  Euphransia JF-Expert Member

  #9
  Feb 17, 2017
  Joined: Jan 26, 2017
  Messages: 944
  Likes Received: 765
  Trophy Points: 180
  Dr. Acha roho mbaya acha wenye. Taaluma yao wachague umelipwa kiasi gani kumchafua Lissu?
   
 10. M

  Msengapavi JF-Expert Member

  #10
  Feb 17, 2017
  Joined: Oct 23, 2008
  Messages: 3,641
  Likes Received: 1,553
  Trophy Points: 280
  Hao TLS hawana katiba na miongozo ya kufuata? Ukawa na Chadema vimeingiaje kwenye mada hii?

  Comments ndiyo mara nyingine zinatufanya wengine tuamini kuwa 1/4 vichaa, labda sababu ya mihadarati!
   
 11. S

  Say no to actors JF-Expert Member

  #11
  Feb 17, 2017
  Joined: Aug 9, 2016
  Messages: 611
  Likes Received: 567
  Trophy Points: 180
  LISSU LISSU LISSU LISSU LISSU LISSU LISSU
   
 12. S

  Say no to actors JF-Expert Member

  #12
  Feb 17, 2017
  Joined: Aug 9, 2016
  Messages: 611
  Likes Received: 567
  Trophy Points: 180
  Amechafuliwaje? Au hujui kusoma watu wa Lumumba mnahaha!
   
 13. HUGO CHAVES

  HUGO CHAVES JF-Expert Member

  #13
  Feb 17, 2017
  Joined: Mar 25, 2011
  Messages: 1,797
  Likes Received: 202
  Trophy Points: 160
  personally sioni shida mh lissu kuwa rais wa TLS as long as anapambania Tanzania yetu,na vinginevyo ushindi kwake sitashangaa kamwe.
   
 14. mangikule

  mangikule JF-Expert Member

  #14
  Feb 17, 2017
  Joined: Jun 11, 2012
  Messages: 2,732
  Likes Received: 752
  Trophy Points: 280
  Mkaifute kwanza hiyo TISS iliyogeuka kwa maslahi ya chama dola bulshit
   
 15. Tukundane

  Tukundane JF-Expert Member

  #15
  Feb 17, 2017
  Joined: Apr 17, 2012
  Messages: 7,319
  Likes Received: 1,581
  Trophy Points: 280
  Tundu lissu anafaa pia kuwa rais wa nchi ya Tanzania.
   
 16. Isanga family

  Isanga family JF-Expert Member

  #16
  Feb 17, 2017
  Joined: Feb 25, 2015
  Messages: 4,017
  Likes Received: 2,761
  Trophy Points: 280
  Lissu ana uwezo mkubwa sana kuliko hata wewe mleta nyuzi hii unawezaje kumkosoa mtu aliekuzidi wa kufikiri na kute na kutetea jambo nimepima uwezo wako kwa hoja yako dhaifu isiyo na mashiko...
   
 17. Mndali ndanyelakakomu

  Mndali ndanyelakakomu JF-Expert Member

  #17
  Feb 17, 2017
  Joined: Dec 14, 2016
  Messages: 6,167
  Likes Received: 12,776
  Trophy Points: 280
  Ujue wengi hatujui kuwa tunapiga kampeni ila tunajua tunachambua hoja
   
 18. c

  chige JF-Expert Member

  #18
  Feb 17, 2017
  Joined: Jul 11, 2016
  Messages: 4,600
  Likes Received: 7,292
  Trophy Points: 280
  Dr.Godbless,

  Mmoja wa viongozi ambao hutakiwi kumtilia maanani ni Mwakyembe! Back then nilidhani Mwakyembe ni very smart kumbe hamna kitu!!!

  Jana ndo kaleta za karne!! Wakati akihojiwa na EATV akadai alitaka kumkamata Agnes Masogange lakini akahamishwa wizara!!

  Mwakyembe anadhani watu tumesahau kwamba Agnes Masogange alirudi Tanzania from South Africa mwaka 2013 wakati Mwakyembe alibadilishwa wizara mwaka 2015... yaani miaka 2 baadae!!! Lakini bado anataka kuaminisha watu kwamba alikuwa na nia ya kumkamata Masogange lakini alishindwa baada ya kuhamishiwa wizara nyingine!!!

  Kati kati ya hicho kiroja akachomekea kingine kwamba mpambanaji wake dhidi ya dawa za kulevya amefungwa kiujanja ujanja ili kumnyamazisha!! Lakini wala hajasema ikiwa alitumia ushawishi wake na uwezo wake kuajiri wakili na kumkatia rufaa! Na wala hajasema amefanya nini kumnusuru huyo mpambanaji baada ya kuwa waziri wa sheria kwa takribani miezi 15 hivi sasa!! Na wala hajasema ikiwa alifikisha hiyo concern yake kwa rais wa sasa ambae tunaambiwa ni mtetezi wa wanyonge!!!

  Kwahiyo, kama vipi wala huna haja ya kumtilia maanani!!!
   
 19. lancanshire

  lancanshire JF-Expert Member

  #19
  Feb 17, 2017
  Joined: Sep 20, 2014
  Messages: 12,452
  Likes Received: 5,970
  Trophy Points: 280
  Mkuu kwa sasa tumeamka na tumesema basi. lissu anatosha for TLS President tumepanga kumpitisha kura zote za Ndio ili tuone CCM wakikifuta chama hiki halafu tukutane mahakamani. Hatuwezi kupelekeshwa kama watoto wadogo sisi
   
 20. Ngushi

  Ngushi JF-Expert Member

  #20
  Feb 17, 2017
  Joined: Jul 8, 2016
  Messages: 4,683
  Likes Received: 7,417
  Trophy Points: 280
  Hebu soma maelezo yake ya ndani halafu rudi urekebishe comment yako
   
Loading...