OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 52,102
- 114,703
Watu lazima waelewe,kwa nini tunaunga mkono yanayomkuta Mh.Makonda kwa dhati.
1.Udhalilishaji kwa watumishi wa umma
Makonda alikuwa kinara wa kudhalilisha watumishi wa umma.Hasa katika operesheni yake ya kufanya mikutano ya hadhara huku akiwaita au kuchukua hatua Kali za kinidhamu pale jukwaani kwa maneno ya kuambiwa tu bila kuwa na ushahidi
Makonda alikuwa ni nambari wani kudharau watumishi kwa lugha za kebehi na kudharau taaluma zao.Mfano aliwahi kusema pale ofisini kwake watumishi wa umma ni wanne tu wengine wote magarasa. Anatutukana sisi kwamba hatuna akili kumbe yeye kabumba vyeti.Huyu ni mdhalilishaji
Kwa hiyo what goes around comes around,Makonda anavuna alichokipanda
Kwa namna ile ile ya kutudhalilisha watumishi akaenda kuwadhalilisha kina Gwajima,Mbowe kumbe amekutana na 'wahuni" wenzie.Amejikuta anabamizwa kiasi cha kushindwa kujitetea akisubiri huruma yetu......Hakuna hiyo muacheni anyooshwe tu,ajitetee mwenyewe
Hata hukumu ya kesi ya kikatiba ya Mh.Mbowe itatusaidia sana watumishi dhidi ya udhalilishaji tunaofanyiwa na wakuu wa mikoa na wilaya.Tunataka watu watuadhibu kwa mujibu wa sheria
2. Ngoswe Penzi kitovu cha Uzembe.
Makonda ametajwa kutumia cheo chake vibaya,ametajwa kutumia ofisi kulazimisha mambo binafsi.Mtu kama huyu ni hatari sana.Hana tofauti na Ngoswe.
Kwa wasio fahamu Ngoswe Penzi kitovu cha uzembe ni hadithi inayofunza watumishi kufanya kazi walizotumwa.Bwana Ngoswe alipewa kazi ya kufanya sensa yeye akaenda kijijini kutafuna mabinti kina Mazoea
Chanzo cha gomvi wa Bwana Makonda Mh.Wema Sepetu kimetajwa kuwa ni mapenzi. Kwamba kuna mmoja analazimisha mapenzi.Hii ni kwa mujibu wa maongezi ya Mama Wema na Steve Mengere
3.Mapambano dhidi ya Ufisadi wa Elimu
Serikali ya awamu ya tano ilikuja na mkakati na matamko mazito dhidi ya watumishi na wore wanaotumia vyeti vya kughushi. Vita hii ilionekana nyepesi kwa wengine. Sasa kwa kuwa huyu kiumbe ni kielelezo cha watumishi waliofoji vyeti,tunataka serikali ichukue hatua.
Sisi tunakomaa kwa kuwa vita hii inapiganwa kibaguzi. Chukulia ingekuwa wewe mtumishi wa RAS Dar Es Salaam umefoji cheti ungenyanyaswaje!!!Sasa kwa nini wengine wapewe mda wa kujipanga wengine tutumbuliwe bila hata kuaga?
3.Uchonganishi wa Makonda
Kaburi la Marehemu Kebwe alikuwa mkurugenzi wa jiji linatikisika.
Makonda ni mchonganishi na hafai kabisa kuwa kiongozi hata wa familia. Sote tulishuhudia akimchongea mkurugenzi kwa Rais kiasi cha rais kumtumbua mzee wa watu hadharani bila kujali utu wake.Nani hafahamu kilichomkuta Mkurugenzi wa Kinondoni Eng.Nati.....
Sasa kwa nini sisi tunapomchongea Makonda tena kwa mambo yenye dalili za kweli tunaonekana tuna chuki.Hapana,what goes around comes around.
Kwa hiyo mambo akiyokuwa akiyafanya Makonda kwa wengine sasa ni wakati wake naye kuburudika nayo ili iwe funzo kwa wengine wenye hulka kama zake
Na watu waelewe kuwa kwa Makonda kutaja majina ya wauza unga hakumpi kinga ya makosa ya jinai aliyofanya au atakayofanya. Hata kama Makonda ungeleta mvua hatuwezi kusema eti kwa kuwa umeleta mvua basi wewe ruksa kutumia cheti cha mtu.Hiyo sheria ya wapi?