Kwanini tunapendelea kujua habari za mtu au kitu usichokipenda?

At Calvary

JF-Expert Member
Aug 22, 2018
4,513
3,554
Salaam wakuu.

Poleni na majukumu ya kulijenga taifa. Pia hongereni kwa kuwa na mchakato huru wa Kampeni za Uchaguzi.

Kuhusiana na mada: Iko hivi, nijichukulie mfano mimi mwenyewe. Sina hakika kwa wengine ila naamini ni wengi tuko hivyo. Mfano mimi napendelea kufuatilia habari za upinzani hasa CHADEMA kuliko CCM.

Huenda sababu yaweza kuwa nataka kufahamu anguko lake! Huo ni mfano.

Sasa swali linasema Swali: Kwanini tu/napendelea kujua habari za mtu au kitu usichokipenda?

Naombeni majibu please!
 
Ukiona hivyo ujue unajishindanisha nae, au unashindanisha Kati ya unachokipenda na usichokipenda
 
Unaependelea ni wewe, majibu sie tunatoa wapi kama sio kwako??
Si kama huwezi jibu ukae kimya tu.

Mbona unapoenda kwa daktari unakuwa unaumwa wewe ila unataka doctor ndio akuambie ni ugonjwa gani.
 
Kuna sababu ila chache ni hizi.

Mtu huyo ni lonely kwa kiswahili labda mpweke hivyo anahitaji mtu wa kushare na interests au kubadilishana vitu tofauti na anachojua juu ya kitu kimoja mnachoshare.

Au mtu huyo anataka challenge akupime kama kweli unajua.

Au anapenda tu kujua interests za watu wengine hivyo kujua jinsi ya kuongea/kuishi nao vipi watu hao.
 
Back
Top Bottom