Kwanini tunamwogopa Lowassa?

R.B

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2012
Posts
6,296
Reaction score
2,578
[h=2][/h]
WAKATI alipokubali kuzungumza na waandishi wa habari kutokea Kilimanjaro Hotel kuhusu mchakato wa kumpata mgombea urais mnamo Machi 14, 1995, Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, alionya mwanzoni mwa hotuba yake kuwa kama waandishi walikuwa wametarajia kuwa katika tukio hilo angetaja majina au jina la mtu anayedhani kuwa anafaa kuwa rais wa Tanzania katika uchaguzi wa mwaka 1995, walikuwa wanekosea.

Alisema kuwa alichokuwa amejiandaa kukifanya ni kuzungumzia sifa ambazo mtu anayepaswa kuwa rais wa Tanzania anapaswa kuwa nazo.

Mwalimu Nyerere alipanga sifa hizi kulingana na changamoto na matatizo ambayo Tanzania, kama taifa, ilikuwa inayapitia wakati huo. Baada ya hotuba hiyo, katika uchaguzi uliofuata, Benjamin Mkapa alichaguliwa kuwa rais akimrithi Ali Hassan mwinyi.

Kama Mkapa alikuwa chaguo zuri au la kulingana na sifa alizozieleza Mwalimu Nyerere bado ni suala la kubishaniwa hadi hii leo. Wapo watu wanaamini kuwa Mkapa ni mmoja wa viongozi waliofanya vizuri sana katika nafasi ya urais wakati kundi jingine likimuona Mkapa kama mtu ambaye ameisababishia nchi matatizo makubwa kutokana na aina ya uongozi wake.

Nimeyakumbuka maneno ya Mwalimu Nyerere kutokana na baadhi ya maoni niliyotumiwa na wasomaji wa safu hii wiki iliyopita.

Katika makala hiyo, niliishauri serikali kufuata ushauri uliowahi kutolewa na Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, katika suala la elimu. Kiufupi, niliiunga mkono hoja ya Lowassa na kuisihi serikali kuiweka elimu kama kipaumbele cha kwanza badala ya kilimo.

Niliandika makala hiyo kwa kuitumia hoja ya Lowassa na wala sikuwa na fikra za kumhusisha Lowassa kama mtu aliyeitoa hoja hiyo. Nilichokiangalia ni hoja yenyewe na si mtoa hoja.

Lakini inaelekea kuna baadhi ya wasomaji ambao walielewa zaidi ya kile nilichokusudia kukieleza katika makala hiyo. Wakiwa na tafsiri zao hizo, baadhi yao walinitumia ujumbe wakinituhumu kuwa katika makala ile nililenga kumpigia debe Lowassa kama mtu anayefaa kuwania urais mwaka 2015. Wengine wakasema kuwa ninajipendekeza kwa Lowassa.

Mmoja aliandika: “Habari ndg Peter? Hakuna cha zaidi cha kuongeza, mnatumia nguvu kubwa kumnadi Lowassa. Tukubaliane kuwa ameshafanya kazi nyingi sasa ni wakati wake wa kupumzika na kula pesa zake. Hafai kuwa rais, kachoka.”

Wakati nikitafakari maudhui ya ujumbe huo kwa lengo la kutaka kumpigia aliyeniandikia ili tuzungumze kwa kina, ukaingia ujumbe mwingine ukisema: “Hivi tumepewa nini na Lowassa tunamfanyia kampeni kiasi hiki?”

Nikaanza kupatwa na wasi wasi kuwa kuna baadhi ya watu hawakusoma kwa makini nilichokiandika na wameamua kuja na tafsiri yao.

Mara ujumbe mwingine ukaingia: “Sijui ni mimi au nini lakini Lowassa huyu si ndiye alikuwa Waziri Mkuu? Ni lipi alilifanya kuhusu elimu japo tuone tu? Si huyu walioanza kuifilisi nchi na kuiingiza kwenye mikataba mibovu. Ni ujiko tu anautafuta na wewe naona kama unajikomba kwake! Hana jipya, lakini unaweza kumbeba.”

Ilipofika hapo nikakata shauri kuwa ingawa sikupanga kuliandikia hili, basi ni vema nitoe ufafanuzi ili tuwekane sawa kuhusiana na Lowassa, urais wa 2015 na ninachokifikiria mimi kuhusiana na suala hilo.

Msimamo wangu hautofautiani na maneno aliyoyatoa Mwalimu Nyerere pale Kilimanjaro Hotel. Naamini kuwa tutafanya kosa kubwa sana iwapo tutaanza kumjadili mtu anayefaa kuwa rais wa nchi mwaka 2015.

Ninaamini kuwa tunachotakiwa kukijadili ni changamoto zinazotukabili kama taifa. Kutokana na changamoto hizo tutapata sifa za mtu anayefaa na baada ya hatua hiyo ndipo tunaweza kuanza kuangalia ni nani anakidhi haja ya sifa hizo.

Kuanza kumjadili mtu hivi sasa wakati hata hatujakubaliana kuhusiana na changamoto na matatizo ya msingi ambayo rais ajaye anapaswa kuyavalia njuga, tutakuwa hatulitendei haki taifa letu.

Kutokana na ninachokiamini sijawahi hata siku moja kuanza kumfikiria mtu fulani kuwa anafaa kuwa rais; si Lowassa au mtu mwingine yeyote yule. Kwa maana hiyo, wale wanaodhani kuwa niliandika makala ile ili kumpigia debe Lowassa au kujikomba kwake, napenda wafahamu kuwa wamekosea.

Na kama wanataka kuthibitisha kuwa wamekosea, nawashauri warudie kuisoma makala ile kwa utulivu ili wanionyesha hata sehemu moja ambapo, hata kwa maudhui tu, nilionyesha kuwa Lowassa anafaa kuwa rais mwaka 2015.

Kwanza hao wanaonilaumu mimi kuwa ninampigia debe Lowassa wanaweza kuwa wanafanya kosa lile lile wanalolipiga vita. Kwa kuwa sikuzungumzia suala la Lowassa na urais, nimeamini kuwa wao ndiyo wanawaza waza sana kuhusiana na Lowassa na urais kiasi kuwa kila wanapoona jina lake limeandikwa, wanasoma kwa ajili ya kutafuta kitu cha kuwalaumu walioandika maandishi hayo.

Ndiyo maana, ingawa sikuzungumzia suala la urais, wao waliweza kuliona hilo.

Kwao hao na wengine wenye msimamo kama huo, naomba kuwaeleza kuwa wanatupotezea muda wenye thamani kubwa sana kwa kutulazimisha kujadili watu. Kuna mambo mengi muhimu ya kujadili likiwamo hili la urais wa 2015.

Lakini, tunaweza kufanya makosa makubwa sana iwapo aina yetu ya mijadala itakuwa ya aina hii ya kuanza kuwaangalia watu badala ya hoja.

Sipingi mtu kuwa na msimamo wa kumuunga fulani mkono katika kuwania urais mwaka 2015. Lakini kama wao wana haki ya kumuunga mkono huyo wanayemuunga mkono, hata kama hawamtaji, kwa nini iwe kosa kwa wengine kumuunga mkono Lowassa?

Nadhani suala siyo kumuunga mkono au kutomuunga mkono Lowassa au mtu mwingine yeyote. Suala tunalopaswa kuliangalia kwa makini ni changamoto zinazotukabili kama nchi na kisha kuorodhesha sifa za mtu anayefaa kukabiliana na changamoto hizo. Sifa hizo ndizo tuzitumie kumpata mtu anyefaa kuwa kiongozi wetu.

Kama kwa kutaja tu suala la elimu kama lilivyozungumzwa na Lowassa kunamaanisha kuwa nimemvalisha Lowassa moja ya sifa za kuwa rais, napenda mambo kadhaa yaeleweke.

Kwanza, sifa ya kuwa rais haitatokana na suala moja tu la elimu. Nchi ina changamoto nyingi zaidi ya elimu. Lakini, msimamo wangu wa kuona kuwa Lowassa analiwakilisha vema suala hili la msisitizo wa elimu haimaanishi kuwa ni yeye tu ndiye mwenye wazo zuri kuliko wote katika suala la elimu.

Niwasihi watanzania wenzangu hawa kuwa wasipofushwe macho na wanasiasa. Iwe ni Lowassa au mwingine yeyote, tunapaswa kufahamu kuwa wote ni wanasiasa na kuwa kipimo tutakachowapimia kinapaswa kuwa sawa.

Inavyoelekea wanamuogopa Lowassa ingawa hajatangaza mwenyewe kuwa atagombea urais. Haya yanayosemwa kuwa atawania urais yanaweza kugeuka baadaye kuwa kweli.

Kama kweli itakuwa hivyo, ushauri wangu kwa hao ambao wanadhani hafai ni kuwa kama wanataka kuuthibitishia umma wa watanzania kuwa Lowassa hafai, basi waje na wagombea wao ambao wana sifa zinazomzidi Lowassa.

Hata mimi, siku nitakapoamua kumuunga mkono mtu fulani, sidhani kama nitajihangaisha na kuangalia upungufu wa wapinzani wake kuwa ndiyo msingi wa kumpa nafasi mgombea ninayemuunga mkono.

Kama kweli nina dhamira ya dhati ya kumfanya mgombea wangu ashinde, basi nitajikita katika kuelezea sifa zake na kwa nini anafaa kuwa rais wa nchi yetu. Kuanza kumponda mpinzani ni dalili za kuonyesha kuwa umeishiwa na hoja za kumsifia mgombea wako.

Napenda kuwathibitishia wasomaji wangu hawa ambao wamenishutumu kuwa ninatumiwa au ninajipendekeza kuwa sina tabia hiyo na wala sitarajii kuwa nayo kwa sababu walionifundisha jinsi ya kuishi hawakunifunda niwe mtu wa kujipendekeza iwapo ninataka mafanikio.
 
KWAHALI ILIVYO NA MATUKIO YANAYOENDELEA TUNAITAJI KIONGOZI MWENYE kuthubutu na mwenye kuchukua maamuzi magumu kwa ajili ya mustakabali wa Taifa



LOWASA ANAWEZA
 

Kama alivyoweza kutangaza mali zake na jinsi alivyozipata,kama alivyoweza kusimamia mchakato wa RICHMOND,Kama alivyoweza kuweka misingi imara ya shule za kata
 
Wewe huyu mtu hasafishiki hata siku moja; wewe ulieandika thread hii unajua kabisa lakini unajipofoa macho kuwa ZEZETA eti hujui kosa la Lowasa, hakuna anayemuogopa mtu muovu, asiependa wanaompinga waishi; Huyu mtu mwaache aendelee kupunguza pesa yetu alieiiba na anayoendelea kuiba kwa kutoa kidogo huko ambako hata Mungu hamsikilizi. Wewe unaemtetea mpe uraisi katika nchi yako sisi wengine hatutakubali MDHAMBI achukue nchi hiii
 
Kwanini tusiwe na utamaduni wa kutoentertain habari za watu ambao kwa namna moja ama nyingine wamehujumu uchumi wa nchi na watu wake kiasi kikubwa na cha kutisha,wameshindwa kujenga au kuboresha misingi ambayo kwayo tutajenga taifa kubwa lenye watu wanaojali maslahi ya nchi na ya umma mpana wa watanzania,hapa tubaki tukijadili adhabu zinazowapasa watu wa namna hii.

Siyo tunapoteza muda wengine wakitetea mpaka povu zinawatoka uovu ambao ilipaswa iwe aibu kwa watu kuutetea kwenye jamii ambazo zinaeshimu miiko ya uongozi,hii si sawa.

Watu wamefanya uhalifu kwa kutumia vyeo/dhamana ambazo tumewapa basi hawa watu si wa kuzungumziwa zungumziwa kama mashujaa fulani kwenye jamii ambayo haijakengeuka kimaadili.Hawa watu walipaswa wawe wamenyongwa na wabakie kuwa mifano mizuri ya nini maana ya kumwadhibu mhalifu anayetumia kofia au mwavuli wa ofisi ya umma ambayo tumemkabidhi kufanya uhalifu wa kuhujumu nchi.

Hapa kwa utamaduni huo mpya tuwe tunajadili maovu yao tu na adhabu wanazostahili,serikali yetu isingekuwa nayo imeoza tokea juu,ingeamua isimame inyonge wawili watatu ya hawa mabig shots,tungeona jinsi watu wanaheshimu ofisi za umma na kujua kwamba zi zao lolote yakiwamo mauti laweza kumtokea.
 
Huo ndio ukweli wenyewe!, anatisha kama jua!, anatetemesha kama tetemeko!, anauwezo kama...., anaogopwa kama .. akiguswa tuu, anarusha kama umegusa umeme!, akifanya harambee fedha zinamiminika kama "strong rooms" za BOT!.

Alopoenda kwa TB Joshua, alielezewa ule mstari wa "Wewe ni mwamba, na juu ya mwamba huu nitalijenga ...langu"
Na akaelezwa kuhusu uwezo wa aliye juu kuwa "Jiwe walilolikataa waashi litafanywa kuwa jiwe kuu la pembeni!"

Yote haya ni bado hajatangaza, watu wanatetemeka, kugwaya gwaya na kuweweseka!, akitangaza jee?!.

NB. As of now, yeye ni "sauti tuu ya mtu aliye nyikani, akiyanyoosha mapito ya "yeye ajaye" "the chosen one!".

Pasco.
 
Umatisha mkuu! Na ukichunguza wangi wao wanao mpinga E. Lowasa ni chuki binafsi na hii ni kutokana na uwezo wake mkubwa kisiasa na kiuongozi pia ambao wanasiasa wengi hawana, wao wame kaa kupiga domo huku action sifuri.
Mungu Mwenyezi ambariki E. Lowasa
 
Anatosha kabisa kuwa mfadhili wa nyumba za ibada zilizokosa maadili ya kiroho.

Kwa kauli hii nimeanza kuingiwa na wasi wasi juu ya upembuzi waki wa mambo,ina maana akija kufanya harambee kanisani kwetu kanisa zima halina maadili? Na kuna post umejibu ukasema aeleze mchakato wa Richmond ulivokua kama mfuatiliaji makini wa siasa za Tanzania utajua tu kuwa kwenye hili alikua msafi ila alitumika tu kama kondoo wa kafala kwani katika vikao vyyao vya chama alimhoji Kikwete kuhusu hili la Richmond kuwa "nilikupigia sim Mh.Rais wakati upo nje ya nchi nikakwambia mkataba wa Richimond tusi usign tuachane nao ila wewe ukanijibu ukaniambia umeshauriwa na katibu mkuu tuendelee nao,cha kushangaza kuna watu wanazunguka nchi nzima na pesa za chama wananiita mi fisadi wakati ukweli unaujua wazi na watu hawa wanaachwa tu"

Toka hayo matamshi ulishawahi kumsikia Nape Nnauye akimuita Lowasa fisadi?

Sisi vijana tena wa upinzani tujitofautishe na wale wa chama tawala kwa kusimamia ukweli na sio propaganda za kuchafua watu bila hata kuwa na ushahidi/uhakika kwa mambo tunayoyasema Mr Ben let's not play their game. Tukienda hivi tutapotezea mwelekeo wananchi na hawatagundua tofauti yetu na wao. Asante
 
Go go go..... EL ur TISHABLE!
 
Haisaidiii kutengeneza majungu huyu jamaa alshajipanga means kwamba Chura hawezi mzuia ng'ombe kunywa maji
 

Amen, well spoken. He had a chance to prove his worthy yet he went on accumulating for himself. he is an adict of wealth
 

Ningekuwa rais ningekuteuwa uwe DPP au Jaji mkuu, period ... nani anabisha
 
Ukisikia wapinzani na hasa CHADEMA wanamshabikia Lowassa ujue wana lao km sio kupandikiza garasa ili waweke King !?!?
R.B. unazijua au kuzisikia Hotuba za Baba wa Taifa?
  • mbona usizitaje alizosema kumhusu Lowassa?
  • mbona hukusema alivyosema kuhusu Majumba ya iliyokuwa msajili na hata zile za S.A.
  • unataka kuniambia hujui hata Mpambe wa baba wa Taifa kule Butiama alipopokea Simu kutoka monduli kuwa aende kusafisha hali ya hewa, mpaka Kawawa kuhusishwa?
  • CC ilipokaa kwa nini waliweka Mitambo ya kuzuia Simu zote zisitoke, ili kujua mchakato unavyoendelea na mpaka leo ni jengo hilo la White House tu huwezi tuma hata msg zitoke nje? wakati wa Kikao.
  • Ni Mhariri gani wa Tanzania Daima aliyeweza kupata Majina ya Kamati ya utekelezaji (Kinana, Mangula, Mwigulu, Zakia nk) saa 5.00 za usiku kabla ya Watu wote hata waliokuwa nje ya milango ya Ukumbi (yaani Gazeti linatoka asubuhi na Majina, Saa nane Majina ni ya kweli na Lowassa hayupo) Basi Muulize A. Kibanda wakati huo alikuwepo kabla ya Mtanzania
Sitashangaa mkianza kupiga debe, kuna jambo maana sijasikia CUF, NCCR, au wagombea buinafsi ila ni hapo tu Nachelea kusema kuna kamkono hapo ambako kameshindwa kuanzia Mkutano Mkuu hadi CC sasa kanakuja kwa gia la Makanisa
Maamuzi ya mwisho ni CC wala sio sisi wachangiaji wa JF Pasco au Ben Saanane
 
Last edited by a moderator:
Umeandika kwa urefu sana lakini kwa Jazba ya kulipa Kisasi kwa waliokupinga ( a.k.a kuwazodoa ) , umehitimisha kwa kuonyesha Mahaba yako kwa Lowasa ! Which is not bad , una uhuru wa kuunga mkono au hata kumpigia debe unayemtaka bila hofu ( japo huamini kama unapiga debe ) , bali ni ukomavu kuzikubali changamoto za watu wengine , hapa siyo kama kanisani kwamba anayeongea ni mtu mmoja tu .
 

Mkuu mimi namkubari sana Lowassa kiutendaji na nakubariana na wewe kuwa issue ya Richmond Lowassa sio muhusika mkuu bali alitumiwa na mkuu wake. Lakini kwa upande mwingine siwalaumu wanaohoji usafi wake mpaka apewe uongozi wa juu,kama yeye aligundua kuwa Richmond haifai na ni mzigo kwa watanzania angesimamia maamuzi yake, kukubari maelekezo ya JK na kisha kukubari uwajibika bungeni ni usaliti kwa watanzania na na kama alithubutu kutusaliti kwa kulinda cheo tu atashindwa kutusaliti tena kwa wawekezaji na kutuingiza kwenye mikataba bubu?
 
Tunamwogopa sana tena sana kwa sababu ni fisadi la ukweli. Hadi VODACOM aliko na hisa ni wezi, sasa akiwa Rais si atahamishia kila kitu kwake?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…