Kwanini tunaibeba DP World kiasi hiki?

UTANGULIZI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, iliyowakilishwa ipasavyo na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi ("Tanzania") na FEMIRATA YA DUBAI, ikiwakilishwa ipasavyo na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Bandari, Forodha na Ukanda Huru ("Dubai");

(Tanzania na Dubai baadaye zinajulikana kama "Wanachama wa Jimbo" (kila moja kama "Chama cha Jimbo"):

(A) KWA KUZINGATIA ziara ya Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Falme za Kiarabu, Dubai Expo 2020 na kikao alichofanya na Mtawala wa Dubai Februari 2022 kuhusu fursa za uwekezaji nchini Tanzania;

(B) KUZINGATIA Mkataba wa Makubaliano (MoU) kati ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na DP World (DPW) uliosainiwa katika ziara ya Mh. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye Maonesho ya Dubai 2020 tarehe 28 Februari, 2022;

(C) KWA KUZINGATIA matakwa yaliyotolewa katika Makubaliano kuhusu maeneo ya ushirikiano kati ya TPA na DPW kwa ajili ya kuendeleza na/au uboreshaji wa uendeshaji na usimamizi wa miundombinu ya kimkakati ya bandari za Bandari ya Tanzania bahari na ziwa, kanda maalum za kiuchumi, hifadhi za usafirishaji na biashara. korido za Serikali ya Tanzania;

(D) KWA KUTAMBUA nia ya Serikali ya Tanzania ya kuhimiza uwekezaji ili kuendeleza na kuboresha utendaji na ufanisi wa bandari za bahari na maziwa ili kuendana na dira ya Serikali na mwenendo wa kimataifa wa huduma za usafiri wa baharini;

P.S.M

Sent using Jamii Forums mobile app
 
MKATABA WA SERIKALI

KATI YA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

NA

EMIRATE YA DUBAI

KUHUSU

USHIRIKIANO WA KIUCHUMI NA KIJAMII KWA MAENDELEO NA KUBORESHA UTENDAJI WA BANDARI ZA BAHARI NA ZIWA TANZANIA.

Oktoba, 2022

P.S.M

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu sitamani kuendelea kusoma hayo madudu wacha niendelee na mambo mengine tu...
 
Ccm wameamua kupanda majukwaani kuutetea kwa nguvu zote, halafu utasikia wanaandaa maandamano kuunga mkono. Waandamanaji mazuzu wataandamana huku hawajalamba hata senti moja, shame on them. Mi kama mwanachama wao kindakindaki hawatanipata kwenye maandamano ya kuunga mkono mkataba huo wa kizuzu kuwahi kutokea duniani
 
Mi kama mwanachama wao kindakindaki hawatanipata kwenye maandamano ya kuunga mkono mkataba huo wa kizuzu kuwahi kutokea duniani


Sent using Jamii Forums mobile app
 
du!!!
 
Billioni walizolipwa wanashindwa namna ya kuzirudisha.
Mzee wa msogizzzz kimyaaaa na yule mwingine wa asili ya sumalia kimyaa kuna jambo. Baba mdogo wa milimani hukoooo kimyaaaa…
Kuna jambo
Ukiona watu wanasogea kwa Maria ujue kuna jambo….
Deal imebumaaaa waachie tu
Tanganyika ni sasa
 
Inauma sana kuona kuwa wabaya wa kwanza wa nchi yetu ni watawala wetu wenyewe na chawa wao - inauma asilani! Tusumbuliwe na kushindana na wa nje, hata watu wetu wa ndani nao watusumbue na kushindana nao??!!

Hivi kwanini tunatesana, tunalitesa taifa na kuvitesa vizazi vijavyo kwa kuukubali utumwa wa kifikra na wa kiuchumi??!!
 
Hembu tuambiane ukweli ni mradi gani Tanzania uliofanywa ambao utaingiza trillioni 27 directly achilia mbali other multiplier, strategically ni win ,ila too emotional individuals watapiga tu makelele. Hata akina Deng Xiaping walionekana wamemsaliti MaO ila wakajenga modern day China muda utaongea .
 
Saingine waliosaini hawakuelewa vizuri kingereza, wamesaini tu.
Hata mimi nina wasiwasi na hilo! Mtu anadai eti DPw watawajengea uwezo TPA kuendesha bandari kisasa, lakini mkataba unataja kuwa DPW watawapa TPA technolojia ya kuendeshea bandari ya majahazi zitakazokuwa chini yao (soma appendix 1, kipengele namba 2 na namba 7 kwa pamoja). Sasa kweli bandari ya majahazi ndo kujengewa uwezo kweli?
 
DPw hata huo muda hawatakuwa nao achilia mbali kuuruhusu uongee
 
Ukiona watu wanasogea kwa Maria ujue kuna jambo….


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…