Kwanini tumuenzi Nyerere kwa kufanya miradi ambayo yeye mwenyewe alishindwa kuifanya?

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
18,305
33,924
Hili swali najiuliza sipati jibu. Kuna umuhimu gani wa kujishughulisha kukimbizana na muda na watu kufanya miradi ambayo Mwalimu Julius Nyerere hakuifanya enzi akiwa madarakani au kuhimiza ifanywe akiwa hai miaka 14 tangu atoke madarakani?

Kuna ulazima wowote wa kufanya kila alichotaka kufanya Mwalimu watanzania wa vizazi kadhaa baada ya yeye kufariki??
 
Nikiongea sana hapa naweza kupigwa mawe.

Ila hoja moja ya kujiuliza kuhusu Nyerere. 'Ni kwanini alishindwa kuweka misingi imara ya demokrasia tangu mwanzo?'

Kama angeliweka misingi imara ya Demokrasia, Tanzania ingekuwa tofauti sana na hii ya sasa.
 
Kufanya miradi kwa lengo la kumuenzi Mtu aliyepita ambae si tija kwa kizazi cha sasa badala ya kufanya miradi iwafaayo kizazi cha sasa hayo ni matumizi mabaya ya Kodi zetu.Nyerere aliishi dunia yake kwa wakati wake na si tija kwa wakati na kizazi cha sasa
Dahh! Aliyejitolea mpaka mshahara na kuacha kazi akipigania tuwe huru ndiyo mnavyomuenzi kwa kumkejeli?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nikiongea sana hapa naweza kupigwa mawe.

Ila hoja moja ya kujiuliza kuhusu Nyerere. 'Ni kwanini alishindwa kuweka misingi imara ya demokrasia tangu mwanzo?'

Kama angeliweka misingi imara ya Demokrasia, Tanzania ingekuwa tofauti sana na hii ya sasa.
Kwani aliyeruhusu vyama vingi kwa kujali masilahi ya taifa alikuwa siyo Nyerere?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dahh! Aliyejitolea mpaka mshahara na kuacha kazi akipigania tuwe huru ndiyo mnavyomuenzi kwa kumkejeli?
Alijitolea mshahara wakati gani na jee huo mshahara wake ulitosha kushughulika na matatizo waliyokuwa nayo watanzania?

Kumbuka sisi wengine ni wafuasi watiifu na kindakindaki wa Falsafa nyingi tu za Mwalimu!!
 
Hili swali najiuliza sipati jibu. Kuna umuhimu gani wa kujishughulisha kukimbizana na muda na watu kufanya miradi ambayo Mwalimu Julius Nyerere hakuifanya enzi akiwa madarakani au kuhimiza ifanywe akiwa hai miaka 14 tangu atoke madarakani?

Kuna ulazima wowote wa kufanya kila alichotaka kufanya Mwalimu watanzania wa vizazi kadhaa baada ya yeye kufariki??
Hivi Mzazi wako mkulima akitumia vijisenti vyake kukusomesha na kununua mashamba makubwa ktk maeneo ambayo hayajaendelezwa Kwa bei nafuu ili wewe kijana wake yaje yakufae mbeleni, akifariki na kukuachia assets hizo utazipuuza kisa tuu Mzazi wako yeye hakupanda ata mti mmoja?
 
Alijitolea mshahara wakati gani na jee huo mshahara wake ulitosha kushughulika na matatizo waliyokuwa nayo watanzania?

Kumbuka sisi wengine ni wafuasi watiifu na kindakindaki wa Falsafa nyingi tu za Mwalimu!!
Heshima na kuenziwa kwa Mwl. Nyerere siyo tu kwa kuanzisha miradi, Bali Ni ushujaa aliouonyesha kuongoza wenzake kuipatia Uhuru nchi yetu, mpaka Sasa tuko katika taifa letu, mpe heshima yake huyo mzee, alihangaika Sana kuliunganisha taifa.

Akaona Ni mda sahihi wa Tanzania kuingia katika vyama vingi na akawezesha Hilo. Bado unaeleza kwa mrengo wa kutothamini lolote alilolifanya ukidai kuwa ilikuwa ya kipindi chake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
akifariki na kukuachia assets hizo utazipuuza kisa tuu Mzazi wako yeye hakupanda ata mti mmoja?
Masuala ya Mzazi na nchi hayafanani. Kwa hii miradi tunayoizungumzia Mwalimu aliacha "Asset" gani inayowezesha kufanyika??
 
Heshima na kuenziwa kwa Mwl. Nyerere siyo tu kwa kuanzisha miradi, Bali Ni ushujaa aliouonyesha kuongoza wenzake kuipatia Uhuru nchi yetu, mpaka Sasa tuko katika taifa letu, mpe heshima yake huyo mzee, alihangaika Sana kuliunganisha taifa.
Kuna mahali nimepingana na haya? Hoja ya Bandiko umeielewa??
 
Nyerere alisema wachache (20%) wasipuuzwe na wasikilizwe, ndipo 1992 mfumo wa vyama vingi ukapitishwa rasmi Tanzania.
Hoja ya Mwalimu kuhusu kuwepo kwa mfumo wa vyama vingi haikujikita katika wingi na uchache!!
 
Wananchi walitaka vyama vingi. CCM ikataka kukataa Mwalimu kwa kutumia falsafa akawashawishi wahafidhina wa CCM wakubali!!
Waliokubali vyama vingi ni asilimia 20% ndipo hapo akaamua kutumia tu ujanjaujanja kuanzisha mfumo wa vyama vingi kwa kuwaweka mapandikizi kwenye vyama vya upinzani.
Kiukweli Demokrasia Tanzania imejengwa katika misingi mibovu kwelikweli.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waliokubali vyama vingi ni asilimia 20% ndipo hapo akaamua kutumia tu ujanjaujanja kuanzisha mfumo wa vyama vingi kwa kuwaweka mapandikizi kwenye vyama vya upinzani.
Kiukweli Demokrasia Tanzania imejengwa katika misingi mibovu kwelikweli.
Hii siyo kweli!!
 
Fuatilia Nyerere alisema Nini baada ya tume ya Nyalali kukusanya maoni ya wananchi ambapo asilimia kubwa walitaka nchi ibaki Chama kimoja,

Nyerere alisema wachache (20%) wasipuuzwe na wasikilizwe, ndipo 1992 mfumo wa vyama vingi ukapitishwa rasmi Tanzania.

Sent using Jamii Forums mobile app
Una bisha tu mkuu, hayo yote ya Nyalali nayafahamu.. ishu kubwa ni kwamba Nyerere hakufanya zaidi ya ilivotakiwa ili kuleta Demokrasia Tanzania.
 
Back
Top Bottom