Kwanini tumbaku inatumika na Mirungi inakataliwa?

Kwanini tumbaku inatumika na Mirungi inakataliwa?

Erick MR

Member
Joined
Nov 11, 2022
Posts
77
Reaction score
166
Nimejaribu kupitia Sheria ya dawa za kulevya Tanzania na nimepata maswali mengi sana kuhusu orodha ya dawa za kulevya inakuaje sigara inayotengenezwa na tumbaku kuruhusiwa kama zao la kibiashara na Mirungi kukataliwa ilihali vyote vina madhara kwa afya ya binadamu.

Hapa kwetu Tanzania nimeshawahi kusikia kijana mmoja huko Tanga 2019 alifungwa miaka 30 kwa kosa la kukutwa na Mirungi na bado utakuta Kuna pahala kiongozi ana himiza ulimaji wa zao la tumbaku

Bado napata ukakasi naombeni hoja zenu Wana jamii ni kigezo kipi kilitumika kupitisha tumbaku kama zao la biashara na kuzuia Mirungi.
 
Unataka mirungi ihalalishwe, hivi wewe huwatakii warangi mema?
 
Shangaa zaidi zao la tumbaku lina bodi yake, chama cha ushirika, wizara ya kilimo inapeka wataalamu wa kilimo cha tumbaku huko wanakolima tumbaku kwa wingi. Mirungi inakatazwa na haina bodi yake ya wataalamu wa kilimo cha mirungi. Mmea mwingine ni bangi nao hauna bodi ya bangi. Ni tumbaku tu, wakati yote ni mimea ya kulevya
 
Umeongea vema mkuu.
Mi sijui umuhimu wa bange na mirungi, lakini napata tabu sana na uhalali wa Tumbaku.

Tumbaku inaangamiza mamilioni ya watu kila mwaka Duniani kote kutokana na sumu iliyobebwa na bidhaa hiyo 'nicotine'.
Biashara ya Tumbaku ni kielelezo kuwa Dunia siyo mahali salama.
Biashara hiyo inaendeshwa na Ma- Tycoon wa Dunia.
Watu hao wamejipanga vilivyo kukabiliana na yeyote mwenye nia ya kuharibu biashara yao hiyo inayofyeka watu kila siku Duniani kote.
 
Tumbaku ni biashara kubwa, na waliowekeza humo tayari wamekita mizizi.. Wanafadhili mirad mingi...
Kukataza tumbaku ni kujiangamiza... DUNIA ina mengi. huenda muuzaj mkubwa wa sigara ndo mfadhili wa PARACETAMOL na ARV
 
Daah tumbaku si ishageuzwa sigara tayari , au anayetaka OG avute zile sigara za Nyota ! Hizi ni biashara za watu aseee
 
Sigara ina madhara ya kiafya ila haileti hallucinations, wakati bangi inaweza tengeneza hallucinations. Hallucinations ndio zinawafanya baadhi ya wavuta bangi kuwa machizi au kujiamini kupita kiasi nk hizi zinafanya mvutaji kuwa hatari kwa jamii yote inayomzunguka.
 
Nimejaribu kupitia Sheria ya dawa za kulevya Tanzania na nimepata maswali mengi sana kuhusu orodha ya dawa za kulevya inakuaje sigara inayotengenezwa na tumbaku kuruhusiwa kama zao la kibiashara na Mirungi kukataliwa ilihali vyote vina madhara kwa afya ya binadamu.

Hapa kwetu Tanzania nimeshawahi kusikia kijana mmoja huko Tanga 2019 alifungwa miaka 30 kwa kosa la kukutwa na Mirungi na bado utakuta Kuna pahala kiongozi ana himiza ulimaji wa zao la tumbaku

Bado napata ukakasi naombeni hoja zenu Wana jamii ni kigezo kipi kilitumika kupitisha tumbaku kama zao la biashara na kuzuia Mirungi.
Tumbaku imehalalishwa kwakuwa walikutwa ishaendelezwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom