Hivi wadau kwanini magonjwa mengi katika mwili wa binadamu yanaambatana na kukosa hamu ya kula, kuanzia minyoo, malaria, typhoid na mengine!!
Je ni mwili unafanya hivyo kujihami na vijidudu vya magonjwa au hivyo vijidudu ndiyo vinasababisha!?
Na ni kipi cha kufanya ili ule kama kawaida ukiwa mgonjwa!!
ukiwa na vijidudu kwenye mwili (infection), mwili unatengeneza chemicals (cytokines) kwenye sehemu ya hiyo infection...hizi cytokines sana sana interlukin 1 na tumor necrosis factor kazi yake kubwa ni kuelekeza seli za kinga za mwili sehemu infection ilipo ilikuzui na kuua hivyo vijidudu!
sasa hizi chemicals ukiacha kazi yake muhimu niliyotaja hapo juu, hua zinaenda kwenye ubongo kwa njia ya damu kwenye sehemu muhimu sana inaitwa hypothalamus
hypothalamus inahusika na kucontrol joto (temperature center) , kucontrol ulaji (satiety center) na kazi nyingine nyingi
zikifika kule zinavuruga mambo, na ni kwa manufaa ya mwili, mfano kitu cha kwanza kitafanya ni kushusha joto la mwili ambalo mwili umezoea, kwahiyo mtu atajihisi homa, nadhani hii inamanufaa kwasababu joto lina wapa vijidudu mazingira ya kukua na kuongezeka so mwili unaamua kushusha ilikuzuia hii
then itavuruga ulaji wa mtu, na utakua unajihisi kutokula , kama unavyojua kwamba vijidudu nao wanahitaji virutubisho kutoka kwenye chakula, mfano madini ya chuma ili waweze kukua na kuongezeka, kwahio mwili unajaribu kuzuia hilo