MeinKempf
JF-Expert Member
- Jun 11, 2013
- 11,094
- 7,225
Kwa heshima na tahadhima naungana na familia na watanzania wote kutoa pole kwa familia , Ndugu na jamaa waliopoteza wapendwa wao kwenye ajali ya basi la shule ya Lucky huko Karatu Arusha. Mola wapumzishe mahala Salama Ndugu zetu waliotangulia mbele za hali.
Nikirudi kwenye mada, Nina maswali ambayo yamenijia kwa mfululizo na kasi ya ajabu sana kuhusu usalama wa abiria wa usafiri maarufu kama dala dala , kwa muda mrefu mpaka muda huu Ninapoandika Uzi huu sijaona sababu au sheria inayoruhusu chombo cha moto kama gari ya kubeba abiria kutembea ukiwa na abiria wasiofunga mkanda .
Je sheria za usalama barabarani zimebadilika siku hizi?? Kiasi kwamba daladala kubeba abiria wasio na mkanda ni sawa, ila dereva peke yake ndo huwa na mkanda (NIT na Kamanda Mpunga tunaomba ufafanuzi wenu).
Je ni sheria ipi inayoruhusu dala dala kupakiza abiria tulioshonana na kusimama kama magunia ya viazi?? (Msiseme labda kwakuwa Nina gari yangu. Hapana, Mimi pia ni mtumia dala dala maarufu)
Kamanda mpunga popote ulipo nakuomba tufanye maamuzi magumu na yenye tija (kama anavyofanya mh. JPM) kwani tukiendelea kulea hali hii kina siku tutakuja kulia na kusaga meno kwa janga kubwa zaid ya hili la Karatu (watu 35 sio idadi ndogo aisee) kufa kwa mkupuo mmoja katika ajali ya barabara ni.
Pia matairi na services za dala dala ni mbovu (kama hakuna anayetakiwa kukagua) maana nguvu kubwa mmeweka kwenye malori ya mchanga na mabasi ya mikoani.
Chonde chonde sheria ya dala dala kupakiza kuzid uwezo wake ifatwe, na pia mikanda na tairi za dala dala ziwe zenye ubora.