Kwanini TCRA hawasajili IMEI numbers za simu kabla ya kuanza kutumika kama ambavyo TRA wanavyosajili chassis numbers za magari?

TCRA wametoa agizo kwamba kila muuza simu lazima asajiliwe. Hii itafanya iwe rahisi kwa simu kusajiliwa kabla ya kuuzwa. Kwa hivyo mkuu usipate shida tatizo lako limetatuliwa
 
Simu nimenunua three years back hilo box lenye IMEI nitakuwa nalo bado tu humo ndani? Kwani kuna technical hindrance gani kwenye kusajili handsets???
Umepewa mfano wa international travellers , amabao wao simu zao zinalazimika kumeza Kila sim card kadhaa kutokana na nchi anayokwenda , Hawa ukimwambia asajili simu basi itakuwa ni usumbufu wa kutosha
Tra wanasajili chassis number kwa sababu hakuna mahala gari Hilo linaweza kutumia namba mbili tofauti na Hadi wanalisajili kinakuwa ni either halijawahi sajiliwa au lilikuwa de registered somewhere .
 
Tra wanasajili chassis number kwa sababu hakuna mahala gari Hilo linaweza kutumia namba mbili tofauti na Hadi wanalisajili kinakuwa ni either halijawahi sajiliwa au lilikuwa de registered somewhere .
Kuna gari za IT zinatoka South Afrika mpaka Tanzani (zingine kutokea Tanzania mpaka Zimbabwe) zinapita nchi ngapi na kote lazima zisajiliwe na idara za customs
 
Umepewa mfano wa international travellers , amabao wao simu zao zinalazimika kumeza Kila sim card kadhaa kutokana na nchi anayokwenda , Hawa ukimwambia asajili simu basi itakuwa ni usumbufu wa kutosha
Usumbufu ndio gharama ya kuishi kwa usalama. Mbona wakati wa operations za Polisi hutangazwa Curfew na watu kulazimika kutotoka nje usiku pasipo kuangalia shughuli za kiuchumi za muhusika. Kwani huu sio usumbufu?

Kuna wakati ni lazima watu wasumbuke kwa maslahi yao wenyewe.
 
Simu nimenunua three years back hilo box lenye IMEI nitakuwa nalo bado tu humo ndani? Kwani kuna technical hindrance gani kwenye kusajili handsets???
Yeah Mimi Nina simu miaka 3 sahizi, box lipo, risiti ipo. Huwa situpi vitu ovyo, box la simu, tv, deki, sijui nini Nina stoo nahifadhi huko
 
Yeah Mimi Nina simu miaka 3 sahizi, box lipo, risiti ipo. Huwa situpi vitu ovyo, box la simu, tv, deki, sijui nini Nina stoo nahifadhi huko
Suala sio kutupa nyaraka hovyo bali ni mambo mengi yanaweza kupelekea vitu hivyo kupotea
 
Kuna gari za IT zinatoka South Afrika mpaka Tanzani (zingine kutokea Tanzania mpaka Zimbabwe) zinapita nchi ngapi na kote lazima zisajiliwe na idara za customs
Gari ya IT haisajiliwi na mamlaka za Kodi Kama ipo on transit , inapita kwa mfumo wa Bond
 
Usumbufu ndio gharama ya kuishi kwa usalama. Mbona wakati wa operations za Polisi hutangazwa Curfew na watu kulazimika kutotoka nje husiku pasipo kuangalia shughuli za kiuchumi za muhusika. Kwani huu sio usumbufu?

Kuna wakati ni lazima watu wasumbuke kwa maslahi yao wenyewe.
Usumbufu ninaongelea ni kuwa ili simu iwe registered na mamlaka ya nchi fulani , inabidi iwe deregistered nchi iliyotoka , ni standard procedure kwa items nyingi hasa magari , huwezi kuwa na kitu kina status mbili kwa sehemu mbili tofauti.
 
Imei ....
FB_IMG_1603269880637.jpeg
 
Kwanini handset isisajiliwe wakati wa kununua pale dukani? Iwe ni compulsory....
Yaani tcra wana uwezo wa kuona IMEI ya simu zote zilizo hewani na kujua simu iko wapi na ni ya nani,, kwahiyo haihitaji process ya kusajili imei ,maana wanaziona automatically,
Tatizo tu,wanashindwa kucontrol,huku africa simu watu wananunua na kubadilishana simu,kiasi kwamba hata wakisajili kwa dizaini hiyo,itawaletea usumbufu wa ku update taarifa kila dakika,
Ndo maana ya ile sheria kwamba ni kosa la jinai kutumia simu isiyo yako,,tatizo hawawezi kucontrol hilo,watu wanabadilishana umiliki wa simu kienyeji na kwa wingi na kila dakika,,
 
Yaani tcra wana uwezo wa kuona IMEI ya simu zote zilizo hewani na kujua simu iko wapi na ni ya nani,, kwahiyo haihitaji process ya kusajili imei ,maana wanaziona automatically,
Mkuu, tatizo lipo kwa ndugu zetu wa Polisi. Kama ukipoteza simu yako na ukaenda kutoa report cha kwanza kukuuliza ni IMEI number wakati wao na TCRA zote ni mamlaka za serikali moja...
 
Mkuu, tatizo lipo kwa ndugu zetu wa Polisi. Kama ukipoteza simu yako na ukaenda kutoa report cha kwanza kukuuliza ni IMEI number wakati wao na TCRA zote ni mamlaka za serikali moja...
Hiyo ni njia ya wao kujipatia kipato, likiwa ni Jambo sensitive imei yako wanaipata tu Wala hawatakuuliza , Ila ukiwa na shida weye ndo wanakutingisha
 
Back
Top Bottom