FikraPevu
JF-Expert Member
- Jan 2, 2010
- 304
- 236
Inaelezwa kuwa vikosi vya jeshi la Tanzania kuendelea kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (Congo DRC) licha ya kupoteza wanajeshi wake 14 katika shambulio dhidi ya waasi, inatajwa kuwa ni hatua ya kudumisha uhusiano wa kibiashara na nchi hiyo.
Wiki iliyopita wanajeshi 14 wa Tanzania na 5 wa Congo DRC waliuwawa na wengine zaidi ya 44 walijeruliwa katika shaumbulio linalotajwa kuwa baya tangu mapigano dhidi ya waasi yaanze katika ukanda wa mashariki mwa nchi hiyo hasa eneo la Kivu ambalo kwa sehemu kubwa linazungukwa na makundi ya waasi.
Kwa mujibu wa Umoja wa Taifa (UN) unasema shambulio hilo lilitokea Desemba 7 mwaka huu katika kambi ya jeshi ya ulinzi wa amani (MONUSCO). Waasi wa kundi la Allied Democratic Forces (ADF) walivamia kambi ndogo iliyopo eneo la daraja la mto Simulike barabara ya kutokea Oicha kwenda Kamanga mpakani mwa Uganda Kaskazini Mashariki ya Wilaya ya Beni, jimbo la Kivu Kaskazini.
Siku chache baada ya shambulio hilo serikali ya Tanzania kupitia Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Luteni Jenerali James Mwakibola alisema shambulio hilo limeleta madhara makubwa lakini kikosi chao kilichopo huko kina uwezo wa kutekeleza majukumu kwa uweledi na umahiri stahiki.
Msimamo huo wa serikali unathibitisha wazi kuwa vikosi hivyo vitaendelea kuwepo katika nchi hiyo ili kurejesha amani na kuimarisha uhusiano uliopo ikiwemo kukuza shughuli za kibiashara baina ya nchi hizo mbili.
Zaidi, soma hapa => Sababu za wanajeshi wa Tanzania kuendelea kulinda amani nchini Congo DRC | FikraPevu