Kwanini Taifa stars na The Cranes watacheza mechi yao Ismailia, Misri?

Uganda kwa story za undugu na ushirikiano zote tunazoambiana wameshindwa kuja kuchezea mechi yao hapa hapa au matengenezo ya uwanja yamekwamisha?
 
Inabidi kama mwandishi uwe unajiridhisha na taarifa unazopewa na source moja. Mimi nimekupa taarifa nyingine kuwa mechi ya marudiano ya Rwanda vs Benin ya March 27 inaenda kufanyikia Huye Stadium ulioko Rwanda.
Smart codetz alikuwa sahihi kwa 100%. Hata media za Rwanda wenyewe waliripoti
Rwanda will play their home game against Benin slated for March 27 in Cotonou after the Confederation of African Football (CAF) announced that Huye Stadium is not qualified yet to host the AFCON qualifiers due to substandard hotels.
Hata hivyo, kwa mujibu wa taarifa za jana kutoka Sportsnews Africa, mechi imerudishwa Kigali.
Halafu wanaendelea
Sasa kama tatizo ni Hotel Falicities, huko Pele Stadium zitatumika hotel zipi?! Hapo ukitafakari utagundua Rwanda walifanya lobbing na ndo maana mechi imerudishwa Kigali kwa sababu hata suala la mechi kuchezwa bila mashabiki wala halina uhusiano na kukosekana kwa hotels za angalau Nyota 4.
 
Aliyesema habari za Rwanda kutokuwa na uwanja siyo Mwanamaji bali ni Smart codetz.

Pia Huye Stadium upo mji wa Butare wakati Kigali Pele Stadium upo Kigali. Unadhani Kigali hakuna 4 star hotel? Pele ni uwanja mpya kwa hiyo labda haujapitia taratibu za ukaguzi ndiyo maana wameuruhusu kama dharura tu kwa condition ya kutokuwa na mashabiki.
 
Aisee
 
Unapenda sana ku-twist mambo! Hoja ni kwamba mlimbishia suala la Kiwanja kufungiwa hadi ukamtaka awe anajiridhisha taarifa anazopewa, na wewe ukadai mechi itapigwa Huye! Lakini kwa tarehe uliyosema hayo, inaonesha wazi Smart codetz alikuwa Sahihi kwa 100% lakini wewe ambae ulijaribu kuaminisha watu kwamba ulikuwa sahihi, kumbe hukuwa sahihi!
 
Msingi wa majadiliano yale ulikuwa ni kama eneo hili la Afrika Mashariki kama kuna uwanja unaoweza kutumia kwa mashindano hayo ya CAF, ndiyo mimi katika kufukunyua nikakuta mechi ya Rwanda itachezewa nyumbani.

Ungeelewa hilo usingejikita kwenye suala la Huye vs Pele stadiums maana wakati tunajadili yale tayari Huye Stadium ulikuwa umeruhusiwa kutumika. Mabadiliko ya uwanja yalikuja baadae.

Na kama ulinisoma vizuri mimi nilikuwa na nia ya kupanua mjadala kwa kuuliza maswali kadhaa. Kwanza suala la ujirani mwema huku tunashindwa kushare viwanja hadi timu mbili kutoka eneo hili tunakwenda kuchezea Misri (tungeweza pia kucheza mechi zote mbili hapa hapa Dar). Pili inakuwaje nchi zetu zinashindwa kumaintain uwanja hata mmoja tu ukawa na standards zinazohitajika muda wote. Kwa kuthibitisha hilo, uliona jana kilichotokea uwanja wa taifa. Mimi nilikuwa zaidi kwenye hoja hizo.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…