kwanini soka la tanzania haliendelei

kwanini soka la tanzania haliendelei

FredKavishe

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2010
Posts
1,090
Reaction score
322
Soka ni mchezo unao pwenda tanzania naweza sema kuliko mchezo mwingine wowote lakini bado mchezo huu wa soka hauwanufainshi vilabu wala wachezaji husika.

Mpira una historia ndefu sana nisingependa kujikita huko leo nataka niongelee kwanini soka letu halina mafanikio hapa nchini kwa miaka zaidi ya 50.angalia uganda wamecheza fainali lakini uwanja haukujaa imagine ndo fainali ingechezwa dar halafu kilimanjaro star ndo inacheza uwanja wote ungejaa.

Tanzania tuna matatizo yafuatayo kwenye soka:
1.Simba na Yanga
Hizi timu mbili ndo tatizo la kwanza kabisa kwenye mpira wa tanzania tukatane tukubali unasadikiwa kila club za simba na yanga zina wanachama zaidi ya milioni 6 je zimewezaje kutumia nguvu hizo za watu mpaka sasa kupata maendeleo ya soka.

Matatizo yao ya simba na yanga
1.Hazina viwanja wa mpira wala vya mazoezi vya kisasa pamoja na kuwa na wanachama milioni 6 na zaidi
2.Hazina academy za soka za kuvutia kutengeneza wachezaji wa miaka ijayo

Mzigo wote wanatupiwa makocha wa stars watengeneze timu haitawezakana hata siku moja timu ya taifa kutengenezwa kocha timu ya taifa inatengenezwa na club ndo msingi imara leo spain wanabeba makombe kutokana na msingia wa kituo cha watoto lamasia.

Kwanini nasema Simba na yanga ni tatizo kwenye maendeleo ya soka pamoja na watu wanavyojaa viwanjani mpaka sasa club hazina pesa hazina nguvu hata Africa zipo zipo.

Mpira bila mashabiki ni bure tuliona Mohamed dewji alijaribu kuja na timu ya Africa lyon lakini akashindwa kutokana na kukosa mashabiki wengi watanzania wanapenda hizi timu mbili utafikiri wamelogewa nazo.

Mpira unahitaji mashabiki ili uweze kuwalipa wachezaji sasa timu nyingi kama za mikoani hazina nguvu kubwa ya wanachama laiti zingekua na nguvu kubwa ya wanachama zingeweza shindana na simba na yanga.

Sasa kuna nguvu ya Azama inakuja unajua nini tajiri atatupa pesa lakini mwishoni atataka timu ianze kumlipa sasa kama haina mashabiki wa kuingia uwanjani kuangalia mpira,wa kulipia ada zao za kila mwezi ni vipi timu itaendelea.

2.Uongozi Mbovu
Soka imekua kama kipitia cha watu wanaotaka ubunge wawe maarafu wanasiasa wengi sasa wanapitia kwenye soka hakuna wale watu wanaoweza kuleta mabadiliko ya kweli ndani ya soka hakuna.

Viongozi wetu wamekosa ubunifu kubuni miradi kama hii
1.Uuzaji jezi ili vilabu vipate pesa wanaachia watu watajirike
2.Kuuza vifaa vingine vya michezo nao wanapewa watu binafsi sio miradi ya timu hebu fikiri yanga na simba zingekua na maduka ya kuuza jezi zao wangekua wanapata sh ngapi.

Suala la mbuyu twite yanga walikosa pesa kubwa sana mbuyu alienda kupokewa na mashabiki wengi sana Airport na kulikua na jezi zenye jina la rage je zingeuzwa kwa mashabiki club ingeingiza sh ngapi madrid walirudisha ela yote waliyo ilipa man utd kwenye usajili wa beckham kwa mauzo na wiki moja tu ya jezi.

Nini kifanyike.
1.Lazima viongozi watambumbue nguvu ya wanachama kama simba na yanga zina wanachama zaidi ya milioni 6 kila mwanachama akilipa 100 ina maana timu itakua na milioni 600 kwa mwezi utashindwa kumlipa kelvin milioni 5 kwa mwezi hauwezi shindwa.

2.Timu zifungue maduka na kuuza vifaa vyao vya michezo

3.Klabu hizi kubwa simba na yanga zijenge academy zao za soka kuanzia miaka 7,miaka 11,miaka 14,miaka 17 tuone kama hatujaenda qatar mwaka 2022 nadhani kucheza world cup.

Ikishindikana ndani ya miaka miwili kufanya hivi tuchukue maamuzi magumu kuvunja Simba na Yanga hapa nchini.kwanini nasema tusivunje hizi timu

1.Kufanya mashabiki wa hizi timu kutafuta timu nyingine za kushangili hii itaondoa usimba na uyanga kwenye soka yetu

2.Kufanya toto kuwa na mashabiki wake wa nyumbani na wanachama wake watakao kufa na timu yao

3.Kulifufua soka letu ambalo kimsingi simba na yanga ndo wameliua kwa miaka nenda rudi.

Maswali ya kujiuliza!!!!
1.Kwanini simba na yanga hazina viwanja vya mpira na vya mazoezi kwa miaka 50

2.Kwanini simba na yanga hazina record sahihi za mashabiki wao

3.Kwanini simba na yanga havina maduka ya kuuza vifaa vyao

4.Kwanini simba na yanga hazina academy za soka mpaka sasa

Kama vyote wameshindwa kwa miaka 50 hivi vilabu haviwezi kutupeleka qatar 2022 vinatudanganya ndo club kubwa hapa nchini lakini ndo club ndogo kabisa kimaendeleo

Tafakari njema

Fred kavishe
 
nimesoma juu juu na naona mawazo yako yamejifunga kwenyo box lile lile dogo la simba na yanga ambapo mtu yeyote mwenye fikra kama hizo daima atahesabika kama kikwazo cha maendeleo yasoka tz, hivyo kajipange upya alafu uje na hoja za kweli za ukuaji wa soka badala la kukopi na kupeste sera za soka la ulaya.
Alafu wakati ukifanya analysis mpya usisahau kujumuisha kigezo kilichotumika kumpa uenyekiti wa kamati ya serengeti boys mh. riz1 na ni matunda gani aliyapata
 
nimesoma juu juu na naona mawazo yako yamejifunga kwenyo box lile lile dogo la simba na yanga ambapo mtu yeyote mwenye fikra kama hizo daima atahesabika kama kikwazo cha maendeleo yasoka tz, hivyo kajipange upya alafu uje na hoja za kweli za ukuaji wa soka badala la kukopi na kupeste sera za soka la ulaya.
Alafu wakati ukifanya analysis mpya usisahau kujumuisha kigezo kilichotumika kumpa uenyekiti wa kamati ya serengeti boys mh. riz1 na ni matunda gani aliyapata

Huwezi zungumzia soka la tz bila simba na yanga ndo kikwazo kikubwa.

Mambo ya riz one kupewa uwenyekiti wa serengeti hausiani kwenye uchambuzi wangu
 
Tanzania ipi?
Tuna Kilimanjaro stars,
Tuna Tanzania bara,
Tuna Zanzibar herous na
Tuna Taifa stars.
Tuna timu nyingi hapa za soka bwana!
 
Nimejikita kwenye soka mkuu

Kwani soka linaongozwa na malaika? Si ni akina Rage hawa hawa ambao tunawaona kwenye siasa? Watafuna nchi ndo wasimamizi wa soka. Huwezi kuitenga soka na siasa za Tz.
 
Back
Top Bottom