Kwanini Simba ya Kimataifa ni tofauti na Simba ya mechi za ndani?

Dabil

JF-Expert Member
Sep 30, 2021
5,885
13,263
Kimataifa unaona Simba inaubonda mwingi tofauti na mechi za ndani, ungesema mechi za ndani ingekuwa inagawa dozi kubwa kubwa lakini ni tofauti struggle ni nyingi, lakini kimataifa mechi ikipigwa unasema hapa sawa.

Mbona timu za nje ndo ngumu,zenye historia na kubwa halafu Simba ikicheza unaona mpira mzuri na sio siri timu zenye makombe Africa zimekufa kwa Mkapa. Lakini kwanini hizi mechi za ndani kwanini ngumu hivi?
 
Msimu uliopita simba ilipoteza mechi moja tu kati ya 30 ilizocheza na ime draw 7. Hapo imeshinda mechi 22

Msimu huu imepoteza mechi moja tu kati ya 10 ilizocheza na ina draw mbili .

Simba ina kombe la ngao ya jamii na ipo fainali mapinduzi cup

Man city last season ka draw 5 kapigwa 5 kati ya 38 , liva msimu huu anaongoza ligi keshabondwa 1 na draw sana .. ligi nyingine utatafuta data mwenyewe

Sasa unapodai mechi za ndani inacheza vibaya sijajua unaangalia nini mkuu ? Hapo Simba ina struggle kivipi ?
 
Kimataifa unaona Simba inaubonda mwingi tofauti na mechi za ndani, ungesema mechi za ndani ingekuwa inagawa dozi kubwa kubwa lakini ni tofauti struggle ni nyingi, lakini kimataifa mechi ikipigwa unasema hapa sawa.

Mbona timu za nje ndo ngumu,zenye historia na kubwa halafu Simba ikicheza unaona mpira mzuri na sio siri timu zenye makombe Africa zimekufa kwa Mkapa. Lakini kwanini hizi mechi za ndani kwanini ngumu hivi?
Labda kama unaongelea misimu ya nyuma, ila kwa msimu huu Smba imeshinda mechi moja tu ya kimataifa (dhidi ya Wydad) katika mechi nane za kimataifa msimu huu walizocheza.
 
Tatizo hamjawahi elewa kua Mashindano ya Makubwa mara Nyingi hua yana sifa moja ya Team kua muoga akiwa Away hsta home.

Kaangalie hata Al Ahly kwenye ligi ana draw hadi na team za mwisho tena kwake...unajua Why?
Kwenye Ligi hakuna kuogopana hakuna kusema nitashinda kwangu nimtoe..Kwenye Ligi kila uwanja una thaman ila hizo Uefa na Caf Champions ni home made oriented games.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom