kwanini si kwa mvuvi huyu?!!!

kabon14

JF-Expert Member
Jun 14, 2016
1,233
867
wp_ss_20170308_0002.png



Ni katika nchi za maziwa makuu, nchi iliyo sifika katika sector ya uvuvi katika pwani ya mashariki na Kati , hii ni baada ya baraza la mawazir kufanya Uchaguzi sahihi wa afisa uvuvi aliyekuwa Na nia thabit ya kupambana na njia haramu za uvuvi katka pwani ile....

Alipopewa dhamana hiyo alionyesha Nia ya dhati katika mapambano hayo, aliitwa mwamba, shujaa na kila jina la kudhihilisha umahili wake.
Vita iliendelea kushika kasi Na kuonyesha mafanikio kwani alifanya uchunguzi wa leseni za wavuvi waliokuwa wakiendelea Na kazi Na alikuwa makini Sana katika kusajili wavuvi wapya kwa kuhakikisha wana sifa na vigezo vya kupewa leseni hizo za uvuvi...

Walioendelea kukaidi walinyang'anywa leseni zao Na kutozwa fain kulingana na sheria za uvuvi haramu, Kuna waliotumikia vifungo pia Kwan uvuvi haramu uliambatanishwa katika makosa ya jinai.

Katika kisiwa cha daring'ombe kulikuwa na mvuvi mashuhuri Sana kuwahi kutokea katika ukanda ule,alifahamika kwa jina la Pondamali Maulaya, mvuvi huyu kwa
muda mfupi baada ya kupewa usajili Na leseni ya uvuvi kutoka kwa afisa uvuvi alifanya kazi kwa juhudi Sana Na kudiliki kwenda hadi Pwani za mbali Sana kuvua samaki...

Alifanikiwa kukifanya kisiwa cha daring'ombe kuwa kisiwa cha maajabu kwa muda mfupi.
Aliuza samaki hadi nga'ambo, lakin cha ajabu mvuvi huyo alikuwa akitumia njia haramu katika kuvua samaki..
(alitumia kemikali hatari Sana Na nyavu haramu)
Hali ambayo ingeweza kuhatarisha species za samaki na hata athar kwa mtumiaji pia..

Watu walipiga kelele Sana kuhusu suala Hilo na hadi afisa uvuvi alizipata habari hizo, lakin hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa, watu wakajiuliza mengi:-

*ina maana afisa uvuvi hakumchunguza vizuri bwana pondamali kabla ya kumpa lesen ya uvuvi?

*ina maana afisa uvuvi hajui kuwa kumuacha bwana pondamali aendelee na uvuvi inaweza kuwa na madhara katka afya zetu kutokana na sumu anazo tumia?


*ina maana afisa uvuvi hawezi kumuwajibisha bwana pondamali?

*ina maana afisa uvuvi anashindwa kuchukua hatua za kisheria dhid ya bwana pondamali Na jamii yake?

Mengi yalijadiliwa , lakin cha ajabu Kuna watu walijitokeza na kupinga uharamu wa matumizi ya kemikali katika uvuvi.!!!
(walidai kikubwa ni samaki na sio njia ya kuvua samaki)

Wazalendo waliendelea kumsihi afisa uvuvi kuchukua hatua lakin hakuonyesha kuwa na kauli tena kuhusu jinai hiyo..

Wengine walisema ni kashfa tu, lakin kwann afisa uvuvi alikosa meno kwa bwana pondamali ikiwa anajua kashfa tu zinatosha kuididimiza wizara ya uvuvi?

Wananchi waliendelea kupiga kelele kila mahali Kwan walishaanza kuona madhara ya samaki wa mvuvi yule..
Kila mtu alikuwa akisubiri kwa hamu kuskia kauli ya afisa uvuvi kuhusu suala hilo huku maisha yakiendelea..!
 
Back
Top Bottom