gemmanuel265
JF-Expert Member
- Feb 16, 2016
- 8,485
- 18,045
Kwa mujibu wa ripoti ya kamati maalum ya kuchunguza masuala ya kisheria na kiuchumi kuhusiana na mchanga wa madini unaosafirishwa nje ya nchi iliyoongozwa na Prof. Nehemiah Eliakim Osoro, ilibaini na kuthibitisha kwa mujibu wa nyaraka na maelezo kutoka ofisi ya Msajili wa Makampuni (BRELA) kuwa kampuni ya Acacia Mining Plc haikusajiliwa (incorporation) nchini Tanzania na wala haina hati ya utambuzi (certificate of compliance) kwa mujibu wa Sheria ya Makampuni, sura ya 212.
Kamati pia ilibaini kuwa kampuni ya Acacia Mining Plc, ambayo inajinasibisha kuwa mmiliki wa Makampuni ya Bulyanhulu Gold Mines Ltd, North Mara Gold Mine Ltd na Pangea Minerals Ltd, haikuwahi kuwasilisha nyaraka wala taarifa yoyote kuonesha kuwa kampuni hiyo ni mmiliki wa Makampuni hayo wala kuwa na hisa katika Makampuni hayo. Kwa kuwa Acacia Mining Plc haina usajili wala utambuzi wa kisheria nchini, hivyo haina sifa ya kupata leseni, kuchimba wala kufanya biashara ya madini nchini Tanzania.
Hivyo basi, kamati ilibaini kuwa kampuni ya Acacia Mining Plc, inafanya biashara ya madini nchini kinyume cha sheria za nchi.
Kamati hiyo pamoja na kubaini kuwa Acacia haina usajili kwa Msajili wa Makampuni (BRELA), pia imetenda makosa mbali mbali ya kijinai yakiwemo ya ukwepaji wa kodi, kutoa taarifa za uongo, kujipatia mali kwa njia ya udanganyifu, uhujumu uchumi na kulisababishia taifa hasara kinyume cha:
i. Vifungu vya 18, 114 na 115 vya sheria ya madini, 2010
ii. Vifungu vya 101 na 106 vya sheria ya kodi ya mapato, 204
iii. Vifungu vya 79 na 82 vya sheria ya usimamizi wa kodi, 2015
iv. Kifungu cha 24 cha sheria ya uwazi na uwajibikaji katika sekta ya madini Tanzania, 2015
v. Kifungu cha 27 cha makosa ya uhujumu uchumi sura ya 200 na
vi. Kifungu cha 203 cha sheria ya usimamizi wa forodha ya jumuiya ya Afrika Mashariki, 204
Lakini pamoja na kamati kubaini makosa hayo kisheria sijawahi kusikia wala kuona serikali ikipeleka shauri mahamani ili kuifungulia kesi ya jinai ya uhujumu uchumi kampuni ya Acacia Mining Plc, na kinyume chake Barrik Gold Mines Ltd walipokwenda kufanya mazungumzo Mh Rais Ikulu, Rais aliwaita wanaume badala ya kutiwa korokoroni kwa kulisababishia taifa hasara kubwa.
Naona hii dhana ya kupambana na ufisadi ina macho, maeneo mengine inakwepa kuchukua hatua za kisheria inabaki kupambana na wazalendo wa nchi hii kwa sababu ya chuki au utofauti wa kiitikadi jambo ambalo mapambano haya hayawezi kufanikiwa pasipo umoja wetu kama taifa, tufanya mambo kwa misingi ya kisheria na siyo kwa mihemko na mbwembwe za kisiasa kwa kutaka huruma za wananchi.