Kwanini serikali isiunde kampuni ya kuchimba madini?

KweliKwanza

JF-Expert Member
Aug 20, 2016
3,517
2,808
Sote tunajua uchimbaji wa madini unafaida kubwa sana kuliko kitu chochote kile duniani kwanini serikali isiunde kampuni ya uchimbaji au kuunganisha matajiri wa Tanzania ili waweze kuwekeza kwenye madini. Ni dhahiri wataendelea na sisi tutaendelea hivyo maendeleo ya nchi yetu yatakuwa makubwa mno.

MD.
Chukulia mfano wazungu au uongozi wa Marekani ungekuwa apa wangekubali kampuni ya nje ndo ichimbe madini?
 
Tatizo la nchi yetu ni usimamizi mbovu na siasa za bongo hatutaweza kuendesha migodi labda tuajiri viongozi wa juu wazungu tunaweza fanikiwa
Unakumbuka viwanda vya sido vilivyo kufa hakukuwa na sababu ya kufa sido maana zilikua zimejitosheleza kabisa hadi viwanda vya kutengeneza vipuli vya viwanda hivyo vilikuwepo Mimi nakumbuka ilikuwa kiwanda kimoja cha sido kiongozi wa juu mfano akiwa mhaya wengine wote wanakua wahaya kibaya zaidi unakuta watu wa familia moja au ukoo mmoja na hivyo kufanya inapotokea mmoja akafanya jambo baya linalosababisha afukuzwe kazi aliye kiongozi ataitwa na uongozi wa familia na kumwambia amsamehe tuu maana akifukuzwa kazi huyo ndugu watakao asilika ni mke na watoto wake
Sido zilikufa kwa njia hiyo
 
Tatizo la Tanzania sio kampuni za kigeni bali ni sisi wenyewe ubinafsi umetujaa.
 
Mgodi wa Tulawaka /biharamulo serikali imejaribu, imeshindwa kabisa kuuendesha ukihadithiwa yaliyokua yanafanyika utazimia!
 
Serikali haiwezi kufanya biashara. Hata marekani hawafanyi hivyo, kinachotakiwa kufanyika ni kuwavutia wawekezaji wasio wababaishaji na kisha kudhibiti na kukusanya kodi stahiki kutoka kwa wawekezaji. Tukumbuke hao wawekezaji wapo kibiashara hawaji kuhubiri injili wanakuja kutafuta faida, na hiyo ipo dunia nzima, kwahiyo lazima serikali iwe na wasimamizi werevu na walio makini.
 
Sote tunajua uchimbaji wa madini unafaida kubwa sana kuliko kitu chochote kile duniani kwanini serikali isiunde kampuni ya uchimbaji au kuunganisha matajiri wa Tanzania ili waweze kuwekeza kwenye madini. Ni dhahiri wataendelea na sisi tutaendelea hivyo maendeleo ya nchi yetu yatakuwa makubwa mno.

MD.
Chukulia mfano wazungu au uongozi wa Marekani ungekuwa apa wangekubali kampuni ya nje ndo ichimbe madini?

Umeona mbali mkuu
 
Haitasaidia kitu.
 
Back
Top Bottom