Kwanini Serikali haitumi fedha za OC Wilayani?

mtzmweusi

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
8,640
8,966
Wakuu habari zenu,

Wilayani siku hizi hatupati Fedha za matumizi mengineyo/Other Charges (OC). Napenda kujua tatizo ni nini na nini kinasababisha serikali haileti fedha za OC maana Halmashauri yetu mara ya mwisho kupokea OC ilikuwa December tuna mrundikano wa madeni makubwa suppliers wanatudai mno hivi hela wanazodai kukusanya zinaenda wapi?
 
Sio nyie tu hata cc huku hatuna fedha tangu December. Nchini Singapore.
 
Tulieni! Haya ndio Maamuzi magumu Rais aache kujenga barabara akuleteeni fedha za mchezo mchezo sijui food and refreshment sijui leave travel sijui office consumables.. hahah Ujenzi naskia hela zimeongezwa mara nne ya bajeti kama vipi pigeni dili utumish mhamie Ujenzi maana kuna watumishi bora wakose Mishahara sio OC!
 
Wakuu habari zenu,

Napenda kujua tatizo ni nini na nini kinasababisha serikali haileti fedha za OC mana halmashauri yetu mara ya mwisho kupokea OC ilikuwa December tuna mrundikano wa madeni makubwa suppliers wanatudai mno hivi hela wanazodai kukusanya zinaenda wapi?
Huwa nawashangaa na kuwaonea huruma wanaoomba tenda za serikali,wanajifilisi wenyewe tu,nafikiri watakuwa na wakati mgumu sana hasa kipindi hiki ambacho serikali haiamini wafanya biashara na inawaharasi
 
Kwahiyo OC unaomba JF jamani,acheni woga ombeni huko waliko zizuia.
 
Poleni kwa kukosa OC kwa muda mrefu.Tuambie pia "Own source" mmekusanya ngapi ? na zimetumikaje? Itapendeza mjadala ukionyesha % ya makusanyo ya "Own Source" na % ya matumizi yake ili Wizara ya fedha iulizwe kuhusu kutowasilisha OC.
 
Wafanyakazi watakoma.....wataisoma namba kwa Mwaka ujao,hakuna OC au

Unafahamu kazi za OC?

Hizo barabara,shule zinajengwaje bila maafisa kwenda kukagua kwa sababu OC hakuna kwahiyo hata ela za mafuta watakosa miradi mingi itajengwa chini ya kiwango halafu watalaumiwa maafisa wa halmashauri.
Viongozi watashindana kutumbua watendaji wa halmashauri kumbe makosa ni ya watoa ela.

Fedha za OC ni muhimu serikali inachotakiwa kufanya ni kudhibiti isitumike vibaya siyo kuacha kupeleka.
 
Unafahamu kazi za OC?

Hizo barabara,shule zinajengwaje bila maafisa kwenda kukagua kwa sababu OC hakuna kwahiyo hata ela za mafuta watakosa miradi mingi itajengwa chini ya kiwango halafu watalaumiwa maafisa wa halmashauri.
Viongozi watashindana kutumbua watendaji wa halmashauri kumbe makosa ni ya watoa ela.

Fedha za OC ni muhimu serikali inachotakiwa kufanya ni kudhibiti isitumike vibaya siyo kuacha kupeleka.
Mradi gani mumeutekeleza kwa kiwango cha kuridhisha wakati mnapewa other charge
 
Ndiyo nafahamu kazi ya OC. Pamoja na kazi nzuri ulizosema hutumika pia kulipana posho za vikao.Kama OC haijaletwa na makusanyo ya ndani yamefanyika mnashindwaje kukagua miradi ya maendeleo?

Halmashauri zote zina wachumi( maafisa mipango) kwa nini hawana mawazo nje ya sanduku la mazoea kupata fedha ?

Wachumi na wahasibu wanaosubiri kuletewa fedha zilizokusanywa na serikali kuu tu wana sababu gani kujiona ni sehemu ya viongozi wa kuongoza serikali za mitaa.

Halmashauri ni serikali kusubiri fedha kutoka serikali kuu ndipo wafanye kazi zao ni sawa na mtoto aliyeoa kusubiri fedha za kuitunza familia yake.
 
Back
Top Bottom