Kwanini SAUT wawe wababe kiasi hiki?

utaratibu wa fine siyo mgeni, tuanze kwenye ngazi za chini kabisa sekondari, hv wewe hujawahi kusikia baraza la mitihani likiwapiga faini walochelewa kulipia ada za mtihani? haya twende kwenye maofisi mengine ya serikali, hv hujawahi kusikia gari la jiji likiwa na kipaza sauti likitangaza kuwa mwisho wa kulipa kodi ya bila faini ni tarehe fulani na baada ya hapo ni faini? haya tutoke huko,tuje kwenye vyuo vya serikali mwalimu nyerere memorial academy, ukichelewa kulipa ada unatozwa faini.sasa chuo hicho kinapata sapoti ya serikali na bado kinatoza faini sembuse chuo kisicho cha serikali ambacho hakina ruzuku toka serikalini? ukiona umeshindwa hamia mnma,udsm au udom ambako wewe unadhani kunaunafuu wa kulipa ada
 
Ni sawa lakini kila jamii inataratibu zake na sheria zinazo eleweka, labda ni kwa sababu hatukumbuki mambo ama hatusomi vitu vya msingi kuhusu chuo. Katika hotuba ya VC Kitima wakati ule (2012) amewahi kusema kuwa chuo (SAUT) jina sheria zake lakini ambazo hazivunji sheria Wala katiba ya jamhuri ya Tanzania. Na kama mlisoma joining instructions form HILI lilibainishwa kwa uzuri sana kwamba kama mwanafunzi atachelewa kujisajiri atatakiwa kukupa faini ya ya Tsh 100,000. Jamani tuache kulalamika kwa vitu ambavyo kama utaulizwa utakosa msingi wa kutetea hoja yako "DICTATORSHIP" kwani hata ya kudailiwa chuoni ulialifiwa hilo, kwa hiyo naona kwa upande wangu hoja na malalamiko mtoa hoja si ya msingi kama alivyo iwasilisha. Naomba kutoa hoja wana SAUT.
 
Sina chuki ila huo n ushaur wajenge kwanza chuo kimoja kieleweke sio kuwa na tamaa! huwaioni UDOM au UDSM vinavyovutia na kuchochea maendeleo sehemu vilipo wao wanaendelea kukumbatia mapor na vichaka katikat ya jiji huku wanakimbilia kuanzisha vyuo mikoani?

Ivi UDSM haina mapori na vichaka? Ukiwa unatikea bondeni unaenda hall 7 lile si pori na chaka au sikuizi wamejenga kwenye mapori yale?
 
Chuki yako haitamdhuru mtu mwingine yeyote isipokuwa personality yako.

Jifunze kusahau mambo ambayo hukuyapenda maishani mwako.

Pia uwe mkweli, hayo uliyoandika hayana ukweli. Uchakachuaji wa matokeo, una ushahidi? Ada hazipandishwi kama unavyodai, na ni za chini kuliko vyuo vyote vya binafsi Tanzania.

Wee tena kaa kmiya hujui side b ya saut nina mifano mingi ya wanafunz walio upgrade matokeo yao na wakatoa mmilion ya hela...vyeti vingi vya kuchonga mtu kaishia mwaka wa kwanza ila alifanya mpango akapata chet kama siye tuliomaliza tena class nzur tu...kwan chanzo cha huyo mkuu wenu aliye-resign baada ya Kitima kuondoka ilikua nn??we nadhan huijui saut vzurii! Waulize waliosomaga hapo wakupe risit za ada uone kama kila mwaka zlikua hazipand!! Usijidai unawasafisha hawana lolote lile.ustake nkaanza kuwataja majina yao na uovu wao. Kiufupi saut wajirekebishe
 
Back
Top Bottom